
umezuka utaratibu wa watu kugeuza mradi wa kujenga vituo vya watoto yatima kama sehemu za kujinufaisha wenyewe na familia zao, huwa sipati picha halisi hasa unapofikia wa kati wa ni wapi mtoto yatima akae? hivi kweli kwa kuwaweka watoto hawa kwenye makambi ndio njia sahihi ya kuwasaidia? (naomba ufafanuzi kidogo toka kwa maafisa ustawi)
hili ongezeko la vitega uchumi binafsi wenyewe wakiita vituo vya kusaida watoto yatima vimeanza kuongezeka na kuwa vingi toka kuibuka kwa NGO, na baadhi ya viongozi wa kistaafu wanakimbilia kuanzisha NGO, wakiwa na lengo la kusogeza siku maana watanzania tuna kipaji cha kuweka vitu katika maandishi hivyo huuandika michanganuo yao na kutuma kwa wafadhiri ili waweze kujinufaisha kupitia migongo ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.
Tuuangalie na utaratibu unao tumiwa na baadhi ya watu wanao kwenda kuwatembelea hawa watoto kwenye vituo vyao, mfano mtu una beba pipi, biskuti na maji eti unaenda kumwangalia mtoto, hivi kweli huyo mtoto ataweza kuishi kwa msaada huo? (naomba msaada wenu maafisa ustawi)
No comments:
Post a Comment