CONTACT US:

CONTACT US:
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com

Sunday, May 3, 2009

AINA GANI YA MAPENZI INADUMU MUDA MREFU?

Mapenzi ni kitu ambacho kina yagusa maisha yetu ya kila siku hivyo basi tunawaletea uchambuzi wa ni aina gani ya mapenzi yanayo dumu kwa muda mrefu.

Watu wengi wanapenda kufatilia habari za mapenzi pamoja na za kwao wenyewe, mapenzi ni hadithi ambayo inaonyesha muonekano, mawazo kuhusu mahusiano. pamoja na hayo habari hizi za mapenzi zimetofautiana kutokana na historia na tamaduni mbalimbali. Wazo la mapenzi kama habari au hadithi linaonyesha kwamba watu hawaangukii kwenye mapenzi ila wana yajenga kwa mfano simulizi nyingi za mapenzi na wapendanao huwa zina mahusiano na mabo wanayo yajua. na mala nyingi simulizi za wapendanao huangukia katika mazingira ya kulijenga penzi lao, utakuta kila mmoja wao anaeleza hadithi (habari ) nzuri ya kuboresha penzi lao. hata kama mwanamke au mwanaume ana mwenza mwingine wa nje hatogusia habari hizo ataleta habari nzuri katika kujenga penzi.

Mapenzi kama ilvyo katika mambo mengine pia yana nguzo zake ambazo zinayafanya yasimame katika muhimili ulio thabiti hivyo basi tuziangalie nguzo kuu za mapenzi ambazo ni;

1; INTIMANCY: hii ni namna ya kujenga mahusiano au mapenzi kwa kujiweka wazi kwa mwenzio hii inasaidia kuleta ukaribu na kuaminiana. Hii ni sehemu ngumu sana katika kujenga mahusiano na mtu umpendaye (mpenzi). unaweza ukakutana na mtu akaziteka ghafla hisia zako za mapenzi, unaweza kufanikiwa kumsalimia ila ukakosa cha kuongea naye. hivyo urafiki wa mahusiano mara nyingi huwa unajengwa kwenye sehemu za kazi, shughuli za wazazi na watu wajamii yako ulio naokaribu. hivyo basi ukifanikiwa kuimudu nguzo hii unakuwa umejijengea mazingira mazuri ya kulijenga penzi lenu.

2;PASSION: hii ni nguzo inayo vutia maana inaongozwa na matamanio ndani ya ndani na mwisho wa yote ni ridhiko na hitaji la mwili. katika hili ndio maana utakuta watu wanajuana siku moja na kufanya mapenzi siku hiyo hiyo, wale ndungu zangu wanao safiri kwa njia ya treni, mabasi na wale wanaonda sehemu za starehe watakuwa wamenipata zaidi.

3; COMMITENT: (majukumu) maamuzi ya kifikira ya kuamua kupenda na kuishi na yule uliye mpenda. mala nyingi katika hatua hii wanaume huwa hawangalii muonekano wa nje wa mwanamke kama mavazi, uzuri n.k.
katika mapenzi wanaume hawazingatii muonekano wa nje bali tabia ndio maana mtu uamua kuchukua jukumu la kuishi na mwanamke kutokana na tabia nzuri.

kuwepo kwa nguzo hizi tatu ndio kunaonesha aina gani ya mapenzi wapendanao waliokuwa nayo. tofauti na haya mabo matatu mapenzi yatakuwa na matatizo.

itaendelea.

No comments:

Post a Comment