
Haina hii ya uvaaji wenyewe wameipa jina la "DUKA" maana yake duka liko wazi, hivyo inamaanisha kuwa huyo dada hapo juu kaiweka bidhaa dukani, kama mama, ama mlezi unavaa mavazi ya aina hii mbele ya jamii tena ya kiafrika na kama haitoshi ni jamii ya kitanzania, hivi tuna wafundisaha nini wanetu walioko shule, walioko mitaani na hata wale ambao wangependa kuwa kama ninyi watakapo kuwa wakubwa.
Umefika wakati wa mwanamke wa kitanzania kuuthamini utu wake na kuacha kuendekeze ulimbukeni wa kuiga uvaaji wa watu wa magharibi, hii itasaidia kuijenga tanzania yenye maadili mema kwa vijana wake.
No comments:
Post a Comment