
VOTE FOR BILAL – PRESIDENCY ISWOSO 2011/12
&
VOTE FOR ROSE MHEREBU – VICE-PRESIDENCY ISWOSO 2011/12
SERA ZETU KWA PAMOJA
MAADHIMIO YA KUJENGA NA KUENDELEZA TAASISI YA USTAWI WA JAMII
1. ELIMU NA MAFUNZO
i. Kuishauri Taasisi kuandaa (DATABASE) mfumo wa uhifadi wa matokeo ya wanafunzi toka hatua za awali hadi matokeo ya mwisho wa semester; hii itarahisisha upatikanaji wa matokeo ya wanafunzi katika hatua zote yenye usahihi kwa wakati wowote ule yatapohitajika. Mfumo ambao kwayo kila muadhili atalazimika kuingiza kumbukumbu za mwanafunzi kuanzia katika hatua ya course work hadi mitihani ya mwisho wa semester.
ii. Kuishauri Taasisi kuandaa utaratibu sare na ratiba maalum ya tests na assignments, kama wafanyavyo Taasisi nyingine kama IFM, CBE n.k
2. KUZITANGAZA FANI ZINAZOTOLEWA NA TAASISI.
i. Kuibua na kukuza ushirikiano wenye na taasisi nyingine mbalimbali ambazo shughuli zake kwa namna moja zina maslahi na Umma wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, ili kurahisisha mafunzo kwa wanafunzi, na kupanua wigo wa wanafunzi wa Taasisi kutamba katika soko la ajira la ndani na la kimataifa.
ii. Kuiunga Taasisi na Mtandao wa Vyuo Vikuu Duniani. Hii itasaidia kutambulika kwa Taasisi ya Ustawi wa Jamii katika wigo wa kimataifa, hali itakayopelekea urahisi wa udahili na udhamini kwa wahitimu wa Taasisi wanaotka kuendelea na elimu katika byuo vikuu vingine vya kimataifa.
3. MICHEZO, BURUDANI NA UTAMADUNI
i. Kuendeleza na kuboresha michezo, burudani na utamaduni ndani ya Taasisi na kukuza ushiriki na ushindi kwa timu zetu katika mashindano ya vyuo vikuu, na mashindano mengine muhimu. Hali itakayosaidia kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi, kuimalisha afya ya mwili na akili kwa wanataasisi, na kuibua mahusiano mema, na hata michezo kama ajira.
4. AFYA, NA MAKAZI
i. kuhakikisha uwepo wa huduma za huduma ya kwanza katika Taasisi ya Ustawi kwanza kwa ajili ya wanafunzi.
ii. kusimamia usafi na upatikanaji wa maji ya kutosha
iii. Kurahisisha upatikanaji wa makazi safi kwa ajili ya wana Taasisi
5. MIKOPO MAWASILIANO, ULINZI NA USALAMA
i. kuimarisha ulinzi na usalama wa mali za wanafunzi
ii. Kuimalisha mfumo wa habari, na mawasiliano utakaorahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu zenye tija kwa wanataasisi kwa wakati unaofaa.
iii. Kuweka mfumo rahisi utawezesha umma wa Taasisi (wanafunzi) kutoa maoni yao muhimu katika kero, ushauri, na maoni katika uendeshaji wa serikali yao
iv. kupunguza urasimu na kuondoa mikingamo katika upatikanaji wa mikopo
No comments:
Post a Comment