CONTACT US:
CONTACT US:
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com
Monday, November 14, 2011
Bi Mkora Alonga Toka Msamvu: Denti Bongo Ana Babu Wa ATM, Denti Mwenzie Wa KuDessa Na Wa Moyoni Mtaani!
Mdau umenena vyema ila umekosea pale ulipoweka percentage kwa sababu hujafanya utafiti uliokupa hiyo data, ungeishia tu kwenye wanawake wengi wana tabia hizo. Huko nyuma nilishawahi kuliongelea hili suala lakini hasa lilihusu wanawake wanaokataa kuolewa na vijana wenzao na kwenda kutembea na waume za watu ambao wamekwishajijenga tayari. Wanasahau kuwa hao waume za watu walikuwa supported na wanawake wenzao mpaka wakafikia kusimama hapo walipo kuwa wenye uwezo wa kuwanunulia magari na kuwajengea majumba au kuwapangia nyumba maeneo ya bei mbaya kama Masaki, Osterbay, Upanga, Mikocheni na Msasani. Wanasahau usemi wa ukiona vinaelea ujue vimeundwa.
Na kwa wanafunzi wa vyuo siku hizi hali ni mbaya wewe unazungumzia huko ughaibuni lakini hata hapa kwetu Bongo ndio inazidi. Wanafunzi wa kike utakuta ana baba mtu mzima mwenye mke na watoto huyu yeye ni ATM tu ya kuhakikisha ana pesa ya kutumbua na kujifanya mutoto wa mujini; kisha ana mwanafunzi mwenzie wa kumpa madesa (sijui siku hizi mnaitaje)huyu kazi yake kumfanyia assignment za shule, kumbuka yeye hana muda wa kufanya assignment kwa sababu yuko busy na biashara ya wanaume na sio kama uwezo huo hana hapana tatizo ni muda. Na mwisho anakuwa na kijana wake anayempenda kwa dhati na ikitokea huyo kijana hajagundua huu mzunguko basi ndio atakayemuoa la akimgundua basi ataishia mtaani.
Na akifika kazini trend ni ile ile pale ofisini atakutana na waume za watu ambao wana pesa za kumwezesha kuendelea kuishi yale maisha yake artificial aliyotoka nayo chuoni, na matokeo yake msichana mwenyewe anakuwa amejifunga kwenye kamba ambayo inamfanya asipate mume wa kumuoa. Hii wasichana wengi hawaijui kwa sababu jinsi wanaume walivyo wakikuona tu unatembea na mume wa mtu basi wewe sio tena wifey materials kwa sababu unaonekana hudhamini ndoa na yeye anaogopa akikuoa utakuja kuisaliti ndoa.
Na zaidi kinachopelekea kuongezeka kwa hayo mambo ya tamaa ni hizi social networks sijui Facebooks na mablogu ambayo wasichana kupeleka mapicha yao ya kuringishiana nani ana amevaa designer's outfit nani anaendesha gari ya kifahari na nani anakaa kwenye mtaa wenye address inayoeleweka, kiujumla ni kama kuna mashindano ya punda na farasi.
Na hao wadada wajameni hawana haja ya kuwaonea wivu mnapokuwa mmeoa wazungu wenu kwani mmetoka mbali kwa shida na raha, mmelala kwenye kachumba kadogo bila heating, mmekula noodles za kupika kwenye microwave, mmekunywa kahawa cheap ya kwenye thrifty shops au 1 pound shop. Sasa ukifika wakati wa hao wadada wa kizungu kula matunda ya kazi yao wao kinawauma nini? Wakiona vimeelea wajue vimeundwa, wakati wenzao walipokuwa wanaunda maisha na nyinyi wao walikuwa wanakula dezo ya vilivyoundwa na wanawake wenzao kwa kutembea na wababa wakubwa waume za watu. Kwa kifupi wamevuna walichopanda na majuto ni mjukuu, wasichana wengi wanasahau kuwa kwa mwanamke kila dakika inayopita na biological time is also ticking.
Kwa kumalizia tu zamani haya yalikuwa zaidi yanafanywa na wanawake lakini siku hizi ni maendeleo hata watoto wakiume wanaopenda dezo hutoka na mijimama mikubwa na kubaki wakiitwa "Serengeti boys". Hili nitaliongelea siku nyingine panapo majaliwa nikipata ka umeme ka kuwasha kwenye komputa yangu huku Msamvu.
chanzo cha habari ni Mjengwa Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment