Ndugu zangu
Kuvunjika kwa ndoa au kutengana kwa wazazi umekua kama mtindo wa kileo bila kujali watoto wataishi maisha gani.
Leo nimeona tuangalie haki anzotakiwa kupata Mtoto anakuwa na wazazi wake wakitengana
Kwa kuzingatia Sheria ya Ndoa, wazazi wanapotengana au wanapotalikiana, mtoto atakuwa
Kupata matunzo na elimu yenye hadhi kama ilivyokuwa kabla wazazi hawajatengana au hawajatalikiana.
Kuishi na mzazi ambaye, kwa maoni ya mahakama, ana uwezo wa kumlea na kumpatia matunzo kwa kiwango kinachostahili kwa ustawi wa mtoto: na
Kumtembelea na kukaa na mzazi mwingine kila anapohitaji, isipokuwa kama mpango huo utaathiri ratiba ya shule au mafunzo kwa mtoto.
Kwa ajili ya kudumisha furaha na amani ya mtoto, mategemeo ni kwamba mtoto mwenye umri chini ya miaka saba ataishi na mama. Hata hivyo, jambo linaweza kupingwa.
Maamuzi yatakayofanywa kwa kuzingatia pingamizi kuwa mtoto asikae na mama, mahakama itaangalia uwezekano wa kumsumbua mtoto katika maisha yake kwa kubadili makazi.
Kwa ushauri zaidi tunaweza kuwasiliana.
Simu: 0686 484866
Email: socialworkertz@yahoo.com
No comments:
Post a Comment