Ndugu zangu
utaratibu wa kufungua mirathi uko wa aina mbili Moja ni Ikiwa marehemu kaacha wosia na ya Pili ni ikiwa marehemu ajaacha wosia.
TARATIBU ZA KUFUNGUA MIRATHI IKIWA MAREHEMU AKUACHA WOSIA
1● Itokeapo kifo,
taarifa ya kifo itolewe na kusajiliwa kwenye ofisi ya mkuu wa Wilaya ndani ya siku (30) thelathini toka kifo kitokee. Kumbuka kupewe hati ya kifo.
2● Kikao cha wana ukoo kifanyike ili kumchagua au kumteua msimamizi wa mirathi na uamuzi huo uwekwe katika dondoo za maandishi.
3● Msimamizi aliyeteuliwa na wanaukoo apeleke maombi ya kupata barua/hati ya usimamizi wa mirathi mahakamani akiambatanisha na;
• Cheti cha kifo, na
• Dondoo za kikao cha wana ukoo kilichomteua muombaji kuwa msimamizi
4●Kiutaratibu Mahakama itatoa taarifa kwa kubandika katika ukuta wa mahakama au gazetini juu ya maombi ya usimamizi wa mirathi na kutoa muda wa siku tisini kuruhusu mtu yeyote kutoa pingamizi kama ana sababu za kufanya hivyo. Kama hakuna pingamizi basi mahakama itatoa barua ya usimamizi wa mirathi kwa mwombaji.
5●Msimamizi wa mirathi hugawa mali ndani ya miezi sita na hatimaye kurejesha mahakamani nakala ya fomu inayoonyesha jinsi mgawo ulivyofanyika na kutiwa sahihi na kila mrithi. Mahakama itafunga jalada.
Barua ya kuomba usimamizi wa mirathi lazima itaje;
a. Familia ya marehemu na anwani zao na ndugu waliokuwa
wakimtegemea.
b. Idadi na aina ya mali iliyoachwa.
c. Juhudi zilizofanyika kuhakikisha kwamba ni kweli marehemu hakuacha wosia.
d. Maelezo kuhusu maskani yake.
Hata hivyo, endapo kunahitajika kufungua mirathi, ni vizuri kwenda mahakamani ili kupata fomu maalum ya kujaza.
Mtu anaweza kufungua mirathi katika mahakama ya mwanzo, Wilaya au hata ya Hakimu Mkazi.
Maombi ya usimamizi wa mirathi lazima yaeleze bayana juu ya yafuatayo;
a. Kiasi na aina ya mali iliyoachwa na marehemu.
b. Majina na anwani za warithi.
c. Sehemu atokayo marehemu na mahali mali zilipo (hii ni muhimu kwani husaidia kuamua ni mahakamani gani stahiki inaweza kupokea maombi ya ufunguzi wa mirathi).
Mawasiliano
Simu : 0686 484866
Email : socialworkertz@yahoo.com
No comments:
Post a Comment