CONTACT US:

CONTACT US:
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com

Thursday, May 7, 2009

CHANZO LA ONGEZEKO LA WATOTO WA MITAANI

Utafiti ulio fanywa na blog ya ustawi wa jamii umebaini kuwa chanzo kikubwa cha ongezeko la watoto wa mitaani ni maelewano mabaya baina ya wanafamilia. utakuta mama mtoto na mawifi zake hawaelewani hivyo mtoto anakuwa anaoteshwa sumu ya kuwa shangazi zake ni watu wabaya kwa kuwa hawapatani na mama yake, na wifi anakuwa hampendi mtoto wa kaka yao kisa ni wifi yao, hivyo ikitokea bahati mbaya mama wa mtoto akafa na yule mtoto akachukuliwa na shangazi zake moja kwa moja huwa anahisi anaenda kuteswa kutokana na yale matukio alio kuwa akiya shuhudia huko nyuma. hata kama mtoto hatoteswa anakuwa anaona njia sahihi ni kukimbia kwenda kuishi sehemu yeyote kuliko kuishi na shangazi zake. na ndio maana ukimuuliza mtoto wa mitaani yeyote chanzo cha yeye kuwa mtaani ni nini atakujibu ni mateso.

NINI KIFANYIKE:
serikali pamoja na asasi zisizo kuwa za serikali zitilie mkazo kuielimisha jamii kwa kutoa elimu maalumu kwa jamii hasa wafiwa jinsi ya kuishi na ndugu walio baki, kuliko kuelekeza nguvu nyingi katika ujenzi wa vituo vya kulelea yatima na watoto wa mitaani. kwa kufanya tutapunguza ongezeko la watoto wa mitaani na mwisho wa siku litakwisha kabisa. nina sisi tiza kuwa vituo vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu sio vizuri na ndio maana hata umoja wa mataifa wanalipiga vita suala hili la kuwa na vituo hivyo.

KAMA ILIVYO KAZI YA MAAFISA USTAWI WA JAMII NI KUELEKEZA WAPI KUNA TATIZO NA NI HATUA GANI ZICHUKULIWE ILI KULITATUA TATIZO ILI KUWEZA KULETA USTAWI WA JAMII, NAAMINI WAHUSIKA WATALIFANYIA KAZI.

NAOMBA KUWASILISHA.

No comments:

Post a Comment