ustawi day

Wednesday, March 14, 2012

RESPONSE LETTER OF THE COMPLAINTS RELATING TO MISSING FUNDS

Dear TASWO Members and Partners.

It is rightly said, no matter how good our intentions and efforts there bound where it is necessary to deal with complaints. This letter is written to all TASWO members and partners as a response of the TASWO Executive Committee to the complaints relating to missing funds collected by TASWO leadership for Gongo la Mboto victims and AGM membership dues. The said complaints were raised by a person who identifies himself/herself TASWO member and has chosen to hide his/her identity.

1)
On the 27th and 28th January 2010, the TASWO Executive Committee held its meeting to deliberate on various issues. We celebrate that the meeting was fully attended by all its office bearers, committee members, TASWO staff and AIHA – Tanzania Country Director, Ms Sally Talike Chalamila, who partially attended the meeting on the 27th January 2012. The thrust of the meeting was geared towards appraising the performance of the association for the year ending 31st March 2012 and establish a planning and budgeting framework for the year starting on 1st April 2012 ending 31st March 2013. The meeting also discussed issues raised by the Ms Sally Talike Chalamila dated 26th January 2012, addressed to TASWO Executive Committee members on their individual capacities. The focus of Ms Chalamila’s letter revolved around an e-mail written by unidentified person claiming to be TASWO member raising issues relating to: a) Missing Gongo la Mboto victim donations b) Missing AGM membership dues. The aforesaid person circulated the e-mail to some TASWO members and its partners as well as donors.

2) The TASWO Executive Committee Meeting carefully and intensively reviewed the contents of the e-mail and discussed the possible sources of information relating to the contents of the e-mail. It noted that a) practical weaknesses in handling the monies for both Gongo la Mboto victims and AGM membership dues, b) money donated for Gongo la Mboto victims was not missing but was banked intact into TASWO Bank Account, and c) the AGM membership dues of the first day of the meeting were given to the TASWO Chairperson who in turn gave to Agape College Cashier for banking to TASWO Account, d) The Agape College Cashier accidentally banked the aforesaid money together with other money of the College to Agape College Account, e) Agape College management discovered the blunder while closing the College Accounts for the year ending 31st December 2011 and reimbursed TASWO money accordingly.


3) The TASWO Executive Committee appreciates the information it has received through a person who for best reason known to himself or herself has chosen to hide his or her identity. It is evident to the Committee that the e-mail writer of having a very close access to confidential information of the association and its partners. It was also plain to the Executive Committee that the e-mail writer purposefully took advantage of the practical weaknesses in handling the funds collected for Gongo la Mboto and AGM membership dues not only to tarnish the image of TASWO leadership, but also to impair the capacity of the association to improve the quality of social work training and strengthening social welfare provision in Tanzania.

4) As narrated in the 2nd and 3rd paragraphs above, the Executive Committee is aware of the negative consequences caused by the identified weakness as magnified by the e-mail writer and improperly of presented to wrong forums. Consequently, it resolved that the money collected for Gongo la Mboto victims to be disbursed to the Dar es Salaam Region Disaster Committee and to accept Agape College money as ratification for a deposit blunder that occurred. It also regrets that the information shared by the e-mail writer by default it implicates the American International Health Alliance – Tanzania and TASWO partners.


5) The TASWO Executive Committee would like to inform all its members and partners that the complaints raised by an anonymous e-mail writer have been democratically discussed and prudent decisions reached to contain negative consequences of the functioning of the association. Accordingly, all TASWO members are urged to continue consolidating on the successes we have so far achieved to revitalize the association through maintaining and enhancing the vibrancy of our programs. This essentially means focusing on TASWO goals and objectives which includes the development of proper tools for administrative and financial management tools as well as succession plans of its leadership.

All in all, the Executive Committee would like to thank the anonymous e-mail writer for indirectly drawing its attention to issues discussed in this letter. The Committee would also like to strongly discourage all its members in using unconstitutional forums that in one way or the other cause inconvenience to various parties and tarnish the image of association and other stakeholders. Consequently, the Executive Committee requests all TASWO members and other stakeholders to accept its apologies associated with improper acquisition and use of information that have caused a lot of inconveniences.
Looking forward for continued cooperation

SAMMY JABAGAMULEMBA
TASWO EXECUTIVE SECRETARY

Monday, March 12, 2012

JE WEWE UMESOMA CHUO CHA USTAWI WA JAMII NA UJAJIUNGA NA TASWO?



Utaratibu wa nijinsi gani ya kujiungs na TASWO utawajia hivi karibuni ila kwa wote wanao hitaji tunaweza kuwasiliana kwa email socialworkertz@yahoo.com

Friday, January 20, 2012

MATOKEO MATOKEO MATOKEO.......................

Kesho Asubuhi matokeo yatatoka kwenye magazeti ya Daily News!

Kama kuna swali wasiliana nasi kwa barua pepe ya socialworkertz@yahoo.com

Tuesday, January 10, 2012

UNAMUAMINI YUPI ZAIDI?



Unaowaona pichani,wote ni wanasiasa.Wote ni vijana.Nape Nnauye(kushoto katika picha) ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM )anayesimamia Itikadi na Uenezi.Kulia ni Mh.John Mnyika(MB) ambaye ni Mkuu wa Habari na Uenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA). Kazi zao zinafanana.Wanaongea na sisi tunawasikiliza.Wanaeneza itikadi na kunadi sera za vyama vyao.

Lakini suala la siasa ni imani.Unaamini kwamba anachokisema yule ni cha kweli na anayo dhamira nzuri kuhusu maendeleo yangu. Sasa wanaposimama hawa wawili kuongea,unamwamini yupi zaidi? Ni kitu gani kinachokufanya umwamini zaidi huyo unayemwamini? Tungependa kupata maoni yako.
Kwa habari zaidi bofya.
NB: Vipima joto hivi vya BC,ni sehemu ya kuhakikisha kwamba viongozi na wananchi wanajua wapi wanaposimama au wanapobidi kusimama kila wakati na sio wakati wa uchaguzi tu.

Wednesday, January 4, 2012

Zachayo S. Shigongo. Atoa somo juu ya majanga yanayoendelea kutokea Tanzania


Baraka pamoja na wote wenye fikra kama zako:

Kuwa Social Worker au kusoma Social Work siyo mchakato wa kuwa kila mahala na kuwa 'kimbele-mbele' wa kukimbia huku na kule kufanya kila kitu. Tatizo na wahanga wa majanga hapa Tanzania la kutopata huduma ipasavyo na kwa haraka ni matokeo ya ubabaishaji au kutojua cha kufanya kwa watu waliopewa dhamana ya kuratibu mwasuala ya majanga na wala siyo la Social Workers kutoonekana kwenye runinga wakitoa 'vijimisaada' ambavyo wengi wanaofanya hivyo hutumia furusa hiyo kujinadi mbele ya camera za waandishi wa habari ili kupata sifa binafsi au kutangaza taasisi/asasi/kampuni zao.

Remember:

1. It is a fallacy to think that standing in front of journalists is equal to working/helping. Most people do that for show up, but serious workers/helpers, in most cases, accomplish thing not even wanting to be recognize. So, when you don't see social workers on front pages of news papers and/or on TVs; don't assume that they are not working/helping. Social Work can never be everywhere. After all they are overwhelmed as we all know that almost everybody in Tanzania is looking upon them to get help.

2. In Disaster Management (if you learned it well); social workers are just part of the Disaster Management Team, with specific roles to play and responsibilities to accomplish which can never be accomplished by other professionals.

Zachayo S. Shigongo ni Mkufunzi wa Chuo Cha Ustawi Wa Jamii.

TAARIFA JUU YA KUJIUNGA NA CHUO CHA USTAWI WA JAMII ZATOKA


Taratibu za kujiunga na chuo cha ustawi wa jamii kwa wale waliokuwa wameomba kujiunga na chuo hicho kwa mwaka huu ni kuwa muda wowote kuanzia sasa tarehe ya taratibu za kusaili na kutambua mazigira itatangazwa.

Na majina ya watu walio chaguliwa yatawaijia hivi punde. endeleea kusoma blog yako ya ustawi wa jamii.

Social workerTZ Team
Dar es salaam
socialworkertz@yahoo.com

KUPANDA KWA NAULI KIGAMBONI NA WIMBO WA GEZA ULOLE TOKA KWA MAGGID MJENGWA


Waziri Magufuli: Na Wa Gezaulole Ya Kigamboni Warudi Tena Mjini?
“ Gezaulole baba, Gezaulole mama ee,
Twendeni Kibugumo na Mwanadilato kwenye makao mapya,
Gezaulole baba, Geza ulole mama eee!”

Ndugu zangu,

Hapa nanukuu gazeti la Mwananchi leo Jumatano; “Majuzi, Dk Magufuli alifanya ziara ya ghafla katika eneo la vivuko hivyo na kuwaambia wananchi waliomzomea kwamba kama wakishindwa kulipa nauli hiyo ya Sh200 ni vyema wakapiga mbizi baharini au kuzunguka Kongowe kuingia katikati ya jiji au warudi vijijini wakalime.”- Mwisho wa kunukuu.

Utotoni katika Dar es Salaam hii, nilishuhudia kwa macho yangu msako wa wazururaji. Niliona jinsi mgambo wa jiji walivyokuwa wakiwadhalilisha vijana na watu wazima kwa kuwakamata, kuwafunga mashati na kuwapandisha kwenye malori tayari kwa safari za kwenda Gezaulole. Kosa lao, walikuwa wakizurura mijini bila kazi. Hivi, anayetafuta kazi atabaki nyumbani kuisubiri, si ni lazima apige mguu kuitafuta? Sijui leo ungefanyika msako wa wazururaji Dar yangehitajika malori mangapi?
Na miaka ile ya sabini tulipokuwa watoto tulisikia hata nyimbo za redioni kuhimiza ‘ wazururaji’ waende kwenye vijiji vipya vilivyoandaliwa na Serikali kama makazi ya ‘ Wazururaji’. Watoto wa enzi hizo huenda tunakumbuka wimbo huu
“ Gezaulole baba, Gezaulole mama ee,
Twendeni Kibugumo na Mwanadilato kwenye makao mapya,
Gezaulole baba, Geza ulole mama eee!”

Kigamboni ya enzi hizo ilikuwa shamba kweli. Wengi wa waliofikishwa huko Gezaulole na vijiji vingine kule Kigamboni wakayaanza maisha mapya ya vijijini. Kuna waliokimbia Gezaulole wakarudi tena mjini au kwenye vijiji vyao vya asili. Kuna waliobaki huko Gezaulole, wakafyeka mapori yao. Wakaanza kilimo, . Wakaizoea hali mpya. Wakajenga familia zao huko.

Ajabu, leo wenye fedha ndio wanaokwenda kuyanunua kwa bei ya hadaa, maeneo ya watoto na wajukuu wa ‘ wazururaji’ wa enzi za Mwalimu. Kuna watoto na wajukuu wa ‘wazururaji’ waliobaki na vieneo vidogo. Miongoni mwao ndio hao wanaofanya shughuli za kusukuma mikokoteni na kuendesha maguta.

Ndio hao, waliokisikia kilio cha kutaka uwepo wa pantoni ya uhakika kwa miaka nenda , miaka rudi. Wamesikia kilio cha kujengewa daraja pia na ahadi zake. Na sasa wanaongezewa nauli ya kivuko kwenda na kurudi mjini.
Ni hivi; mkazi wa Magomeni hata kama hana nauli anaweza kutembea kwa miguu kukatisha Jangwani na akamwona mgonjwa wake Muhimbili, au kwenda kuhangaikia kibarua Kariakoo. Na jioni ikifika, hata kama hana nauli ya Daladala, atakatisha Jangwani na kufika Magomeni kwenye chumba chake cha kupanga.

Lakini, mkazi wa Kigamboni kama hana nauli ya mia tatu ya pantoni na kama anataka kuvuka kwenda kumwona mgonjwa wake Muhimbili au kuhangaikia kibarua Kariakoo ana mawili, kwa mujibu wa Magufuli; ama apige mbizi au azungukie Kongowe, kwa miguu, mwendo wa nusu siku kama si siku nzima. Na hapa ndipo ilipo hoja ya msingi ya kumfikiria mtu wa kawaida wa Kigamboni, Gezaulole na kwingineko ng’ambo ya pili ya bahari.

Vinginevyo, kwa kusema kuwa asiye na nauli arudi kijijini akalime ina maana pia, kuwa kuishi Jangwani, Mburahati na Mabibo kunaweza kuwa na nafuu zaidi kwa mtu wa Kigamboni mwenye hali ngumu kiuchumi. Kwamba hatimaye tunawaambia watoto na wajukuu wa ‘ wazururaji’ wa enzi za Mwalimu;
“Rudini mjini’. Na wimbo ule leo labda ungeimbwa hivi;

“ Mburahati mama, Mburahati baba ee,
Rudini Jangwani, na Mwananyamala kwenye maisha bora!”
Haki ya Mungu!

Maggid Mjengwa,
Msamvu, Morogoro.

Thursday, December 8, 2011

CHUO CHA USTAWI WA JAMII NDANI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU




PICHA HIZI ZIMEPIGWA KWENYE MAONYESHO YA MIAKA 50 YA UHURU YANAYO ENDELEA KWENYE VIWANJA VYA MAONYESHO YA KIBIASHARA SABASABA

Friday, November 25, 2011

VIWANJA VYA USTAWI WA JAMII KUWAKA MOTO KESHO


Baadhi ya wasanii watakaofanya makamuzi siku ya Jumamosi

SHOO ya uzinduzi wa mix-tape ya Anti Virus inazidi kubamba, upo uwezekano ikajaza nyomi ambalo halijawahi kutokea kutokana na ahadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu kwamba watakodi mabasi kwenda kwenye viwanja vya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar.

Anti Virus itasababishwa na Vinega Novemba 26, 2011, kuanzia saa 12 jioni mpaka 6:00 usiku na katika kuhakikisha wanashuhudia makamuzi ya maana, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, wameahidi kukodi mabasi matatu ya kuwasafirisha kwenda kwenye shoo hiyo.

Wanafunzi wa Tumaini Dar, wamemuandikia SMS, kinega mkuu ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, wakimueleza kuwa madenti wa vyuo vikuu wapo naye katika harakati za kuwakomboa wasanii wa muziki wa kizazi kipya.

“Wanakuita Sugu… Sugu… Sugu…Sugu! Kaka sisi wanafunzi wa Tumaini University ya DSM, tumeamua kukodi mabasi matatu ya UDA ili kuja katika shoo yako na Vinega hapo Viwanja vya Ustawi wa Jamii,” ilisomeka SMS hiyo.

Mratibu wa shoo hiyo, Fred Mariki Mkoloni alisema kuwa jukwaa na muziki (sound) ni vya kiwango cha juu na kwamba kinachosubiriwa siku hiyo ni wasanii Anselm Ngaiza ‘Soggy Dog,’ Suma G, Mapacha, Dani Msimamo na wengine kibao wakiongozwa na Sugu kuwasha moto wa gesi.

Thursday, November 24, 2011

UKATILI WA KUTISHA



Jeshi la polisi kanda maalum ya Temeke jijini Dar linamsaka kwa udi na uvumba mwanamke aliyetambulika kwa jina Frolentina Otto 42 maarufu kama Mama Twala kwa tuhuma za kuchoma moto nyumba ya mamake mdogo na kusababisha mtoto mdogo anaye fahamika kwa jina la Jacqueline Rides (11) kuungua vibaya mwilini.

Chanzo Gazeti la sani jumatano tarehe 23/11/2011 toleo namba 862

Wednesday, November 23, 2011

Tanzania Haitalazimishwa Kukubali Haki za Mashoga!!


Tanzania stands firm on aid-gay rights spat with UK
By Fumbuka Ng'wanakilala | Reuters – Fri, Nov 4, 2011

DAR ES SALAAM (Reuters) - Tanzania has become the latest African government to say it will not legalise homosexuality even if that means it loses substantial financial aid from Britain.
Government officials reacted strongly to Prime Minister David Cameron's threat to cut aid to countries that deny gay rights.

"Tanzania will never accept Cameron's proposal because we have our own moral values. Homosexuality is not part of our culture and we will never legalise it," foreign affairs minister Bernard Membe was quoted as saying by Tanzania's Guardian newspaper.

"We are not ready to allow any rich nation to give us aid based on unacceptable conditions simply because we are poor. If we are denied aid by one country, it will not affect the economic status of this nation and we can do without UK aid."

Tanzania, a former British colony and one of Africa's biggest per capita aid recipients, received $453 million (282 million pounds) of aid for its 2011/12 budget, with Britain the largest provider of general budget support.


Ghana's President John Atta Mills said Wednesday his government would never legalise homosexuality. Uganda has also reacted strongly to Cameron's comments.

The Department for International Development (DFID) gave Tanzania 144 million pounds in aid in 2009/10 and has pledged to spend an average of 161 million pounds per year in Tanzania until 2015.

Homosexuality is a serious criminal offence in Tanzania, punishable by imprisonment, but no one has been prosecuted.

"We cannot be directed by the United Kingdom to do things that are against our set laws, culture and regulations," Membe was quoted as saying.

Zanzibar President Ali Mohamed Shein also rejected the British demands for gay rights to be respected in Tanzania.

"We have strong Islamic and Zanzibari culture that abhors gay and lesbian activities, and to anyone who tells us that development support is linked to accepting this we are saying no," Shein told journalists Thursday.
Zanzibar, Tanzania's semi-autonomous archipelago, enacted a law in 2004 banning homosexual relations. Male offenders face more jail time, up to 25 years, than convicted women.

Homosexuality is illegal in 37 African countries, and rights groups say gays are often the targets of violent hate campaigns.

(Additional reporting by Ally Saleh in Zanzibar; Editing by Richard Lough and Robert Woodward)

IMANI ZA KUVUNJA NAZI NJIA PANDA BADO ZINAENDELEA




Picha kama zilivyo kutwa na mpiga picha wetu

Tuesday, November 22, 2011

AFISA USTAWI WA JAMII KOROGWE APONGEZWA

Mhariri,
SINA shaka na kujitokeza kwangu hadharani kupitia gazeti hili kutoa maoni yangu kwa nia ya kumshukuru na kumuenzi afisa ustawi wa jamii wilayani kwetu, Korogwe, Tanga.

Kwa hakika ni kwa jinsi ambavyo anatumikia jamii tangu nilipoanza kumuona, yapata miaka kumi iliyopita.
Kama tunavyofahamu, majukumu ya ustawi wa jamii katika kusimamia, kuelekeza na kuhakikisha malezi ya watoto yanakidhi kiwango hasa kwa wanandoa/ marafiki wanapohitirafiana, kuhusu suala zima la matunzo ya watoto, ni kazi nzito.

Imekuwa kama kawaida kwa sisi hasa kina baba kuwaachia mzigo mkubwa wa malezi kinamama kwa visingizio vingi.
Baadhi ya kina mama waelewa hukimibilia katika idara hii, ndipo ninapommiminia sifa lukuki afisa huyu kwa ushahidi ufuatao.
Wakati mmoja mwaka 2004, nilishuhudia kisa kimoja cha afisa wa serikali tena katika taasisi nyeti sana, mwenye cheo kikubwa alipopelekwa kwake na mama ambaye ni mkazi wa kijijini kwetu.

Afisa huyu hakujali cheo kikubwa cha mwanaume huyo wala uwezo wake wa kifedha, alisimama kidete kutetea haki za mwanamke na mtoto husika mpaka wakatendewa haki kwa mujibu wa taratibu.

Ni mengi amefanya ofisa huyo, si vyema kutomshukuru angalau kwa njia hii, ili kumtia moyo aendelee kufanya hivyo kwa wengine wenye matatizo kama hayo huku akifahamu kuwa jamii iliyomzunguka ipo pamoja naye, na inamkubali.

Naamini viongozi wengine hawana budi kuiga kwa utendaji wa kazi wa ofisa huyo na wote wangekuwa hivi tungekuwa mbali kimaendeleo na katika kuondoa kero za wananchi.

CHANZO MWANANCHI Friday, 18 November 2011 09:25

Monday, November 21, 2011

UMASIKINI WA TANZANIA NA MAENDELEO MABOVU YA ELIMU


SHULE ya Msingi Kitete iliyopo katika kata ya Uchindile, Tarafa ya Mlimba wilayani Kilorombero mkoani Morogoro yenye walimu wawili tu na wanafunzi 29 ipo katika mazingira yanayoashiria imetelekezwa.

Shule hiyo iliyoanzishwa kwake mwaka 1976 ipo zaidi ya kilomita 150 kutoka Kilombero na kilomita zaidi ya 125 kutoka Mafinga, mkoani Iringa.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idd Mdaba alisema tangu ahamishiwe katika shule hiyo mwaka 2008 kwa ahadi kwamba angehamishiwa shule nyingine baada ya miaka mitatu, amekuwa akifundisha mwenyewe wanafunzi wa madarasa yote yaliyopo katika shule hiyo.


“Hata hivyo nashukuru mzigo huo umepungua mwezi mmoja tu uliopita baada ya kuletewa mwalimu mwingine mmoja kutoka wilayani Geita ,” alisema huku Mwalimu huyo Juma Deke akidai kujutia uamuzi wa kuomba uhamisho kutoka Geita ili ahamie mkoani kwake Morogoro kwani hakujua kama angepangiwa shule kama hiyo.
Alisema mbali na shule hiyo kutokuwa na vifaa vya kufundishia na kujifunzia, ofisi ndogo ya mwalimu na madarasa yake matatu yaliyopo, hayajasakafiwa chini na kuta zake, hakuna madirisha na milango na yote kwa ujumla wake yana madawati yasiozidi 20.
Mdaba alisema mazingira hayo yameifanya shule hiyo kukosa wanafunzi wa darasa la kwanza, la tatu na la tano hadi la saba hivi sasa baada ya waliopaswa kuwa wanafunzi wa madarasa hayo kutosajiliwa mwaka wa kwanza wa masomo yao ya darasa la kwanza


Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitete iliyopo katika kata ya Uchindile wilayani Kilombero, Idd Mdaba akitoka kwenye ofisi yake kama anavyoonekana.
Source:Frank Leonard


Hili ni moja ya darasa la shule ya msingi Kitete iliyopo kata ya Uchindile wilayani Kilombero linavyoonekana kwa ndani. Shule hii ina walimu wawili na wanafunzi 29 tu kwasababu ya mazingira yake

WATANZANIA WANAOISHI UJERUMANI ! WAANZA KWA KASI! KUSHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA


Miaka ya 50 ya uhuru wa Tanzania bara,kusherekewa kwa Kishindo Ujerumani !
Sherehe ambazo zitaambatana na ufunguzi wa Umoja wa Watanzia Ujerumani (UTU)
siku ya Jumamosi 10-December-2011 Mjini Berlin

Saturday, November 19, 2011

CHANGA MOTO YA UKIMWI NA UTAMADUNI TOKA KWA MDAU WETU JONIA BWAKEA


Pichani ni dada Jonia Bwakea

Watanzani wenzangu ukimwi unawauwa waafrika utamaduni hauruhusu kuzungumzia sexuality lakini ukweli the popluation structure esp young people 65% ni sexualy active na wengi wanafanya unsafe sex na mabya zaidi walio wengi wanmultiple sexual partners. Tufike sehemu tuweke mambo hadharani na vijana tuthamini maisha and no one is responsible of our actions expect ourselves.

watu katika jamii waongee na vijana wazazi walezi juu ya ukimwi maana ni hatari....mtu kama unjijua uwezi kujizuia au kuwa mwaminifu tumia condom na huo ndo ukweli la cvyo tutakwisha. Maadili yetu tunaambiwa tusubiri mapaka ndoa na dini zote zasema hivyo lakini sasa ni kwamba ABSTINENCE is less practical therefore what comes next? i dnt encourage people kufanya ngono b4 marriage but let us talk of the reality.....kama hatujilindi tujue kuwa twafaaaa

lakini pia tujiulize wangapi kati yetu tunapoanzisha mahusiano tunaenda kupima afya zetu? wanawake au wanaume wangapi wan ujasiri huo? LET US THINK TWICE

Takwimu zinaonyesha ukimwi umebakia kuwa ugonjwa wa watu wa nchi za masikini ikiwemo Afrika na hata matibabu yake hasa kwa walioathirika ..read UNAIDS 2010 HID AIDS report....

Culture and Poverty and IGNORANCE are hindrance against HIV combat in Africa.

Thursday, November 17, 2011

Mtoto huyu akifa, sababu ni mil. 3



Mtoto Pascal Tano akiwa na mama yake, Jane Leo, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

HII inauma sana, mtoto anaumwa, mzazi amegundua tatizo linalomsumbua lakini fedha ya matibabu hakuna. Wapo wapi waliojaliwa na Mungu kumuokoa malaika huyu wa Mungu?

Mtoto Pascal Tano, mwenye umri wa miaka mitano, ana hali mbaya, amebainika kuwa na matundu kwenye mishipa ya damu lakini badala ya kupata matibabu, kwa sasa yupo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa sababu mama yake hana fedha za kumgharamia.

Jane Leo, mama mzazi wa Pascal aliliambia Uwazi kuwa mwanaye alifanyiwa kipimo cha OGD kwenye Hospitali ya Aga Khan na kubainika kwamba ana matundu katika mshipa wa damu tumboni.

Alisema, baada ya vipimo kubaini hivyo, ilitakiwa achomwe sindano sita ambazo kila moja gharama yake ni shilingi 460,000 pamoja na dawa ya usingizi chupa sita, ambazo zinagharimu shilingi 50,000 kila moja.

“Jumla ya fedha zote zinazohitajika ni shilingi 3,100,000. Hizo fedha nitazipata wapi mimi maskini ya Mungu? Nina mawazo mengi juu ya afya ya mtoto wangu,” alisema Jane.

MTOTO AMETESEKA!
Kwa mujibu wa Jane, Pascal alianza kuugua tangu akiwa na umri wa miezi tisa, hali ambayo ilimlazimu kutembea hospitali mbalimbali kutafuta matibabu.

Jane, mkazi wa Kijiji cha Statike, Wilaya ya Mpanda, Rukwa alisema: “Tatizo lilianza kwa homa za mara kwa mara, tumbo kujaa, kukohoa na kutapika damu. Nilimpeleka Hospitali ya Mpanda lakini hawakugundua ugonjwa. Hali ilizidi kuwa mbaya, akaongezewa damu lita nne lakini wapi.

“Kimsingi aliongezewa damu mara nyingi. Akiwa na miaka mitatu nilimpeleka Hospitali ya Mkoa wa Singida, madaktari wakasema anaumwa kifua kikuu. Tulipewa dawa lakini hazikusaidia. Pamoja na uhaba wa fedha, nilimpeleka Hospitali ya Mkoa wa Tanga akiwa anatapika damu mara kwa mara lakini hatukupata mabadiliko.

“Madaktari wa Tanga walishauri nimpeleke Muhimbili, Agosti 26, mwaka huu nilifika Dar. Moja kwa moja, nikaenda Muhimbili, akapigwa x-ray, ugonjwa haukuonekana. Nikaandikiwa kipimo cha OGD ambacho kilifanyika Aga Khan ndipo lilipobainika tatizo la matundu kwenye mshipa wa damu tumboni.

“Kipindi chote nazunguka mwenyewe kwa sababu mume wangu amebaki Mpanda, anamlea mtoto wetu mdogo mwenye umri wa miaka miwili ambaye anaitwa Januari. Hapa nilipo sina mbele wala nyuma, naomba Watanzania wanisaidie kumpatia matibabu mtoto wangu na Mungu atawalipa.

“Watanzania wasikie kilio changu, wanaoguswa na tatizo la ugonjwa wa mwanangu na kuwa na lengo la kuokoa maisha yake wanisaidie kwa kuwasiliana na mimi. Namba yangu ni 0753-673815 au hata wakiniulizia Muhimbili, watanipata.”

Shoo ya Sugu na Vinega Ustawi yabamba kitaa


Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

KITAA kimechafuka na kila mtu kwa sasa haambiwi kitu kuhusu shoo ya Burudani kwa Mashabiki, Muziki Unalipa ambayo itafanyika Novemba 26, 2011 kwenye Uwanja wa Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar es Salaam.

Shoo hiyo, ‘itagemuliwa’ na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, huku wakongwe Haroun Kahena ‘Inspector Haroun’ na Karama Bakari ‘Luteni Kalama’ wakiwa na dhamira ya kuthibitisha kwamba Gangwe Mob Bongo jukwaani ni sawa na G Unit Marekani.

Shujaa wa Kundi la Wagosi wa Kaya, Fred Maliki ‘Mkoloni’, Anselm Ngaiza ‘Soggy Dog’ na mwana Hot Pot Family mwenzake, Suma G, Mapacha, Dani Msimamo, G Solo, Rama Dee, Peen Lawyer, Adili Mkwela ‘Hisabati’, D wa Geto, Magazijuto, Coin, LWP ‘Majitu’ na wengine kibao.

Uchunguzi umebaini kuwa gumzo kuhusu shoo hiyo imeshika mbaya kitaani, huku ubunifu wa matangazo na viwango vya Vinega wa Anti Virus vikiwa ni kielelezo cha kumfanya kila Mtanzania aone tamasha hilo si la kukosa.

Mratibu wa shoo hiyo, Mkoloni anapatikana kwa namba 0719 690 100, hivyo maelezo kuhusu utaratibu wote kwa jumla, yanapatikana kwake.

UMASIKINI WA WATANZANIA NA MAADHIMSHO YA MIAKA 50

Wednesday, November 16, 2011

KUBAKWA + KUCHOMWA NA PASI = MATESO MARA 2


katika hali isiyo kuwa ya kawaida na ya kusikitisha, mtoto ambaye wiki iliyo pita alilipotiwa na gazeti la sani kuwa katekwa na mwanaume ambaye bado hajafahamika kisha kubakwa usiku kucha hali iliyo mfanya aumizwe vibay sehemu za siri, amepatwa na janga jingine baada ya mama yake mzazi kumuadhibu kwa kumchoma na pasi ili amtaje mbakaji huyo.

wakiongea kwa masikitiko makubwa majirani wa mama wa mtoto huyo aliyefahamika kwa jina moja la Aziza, wakazi wa kinondoni mkwajuni jijini wamesema wamesikitishwa na tukio hilo kwani ni lakinyama na linapaswa kupigiwa kelele.

Mama huyo inadaiwa alianza kumshushia kipigo mtoto wake huku akiwa ameichomeka pasi kwenye umeme hadi alipooona imekuwa nyekundu na kumkandamiza nayo kwenye paja kwa dakika kadhaa, akimtaka amtaje mwanaume aliye mbaka.

Habari zaid zinasema kwamba baada ya kumpa kipigo hicho alimuamuru mtoto huyo alale na asitoke nje hadi atakapopona, hata hivyo siri ilivuja baada ya majirani kugundua ukatili huo.

wanahabari wa gazeti la sani walifika nyumbani hapo na kumkuta mtoto akiwa katika hali mbaaya, alikiri kupigwa na mama yake na akaomba baba yake popote alipo amchukue.

Alimtaja baba yake kwa majina ya Juma Selemani na kudai anaishi mjini Arusha, aipo ulizwa lini ilikuwa mara ya mwisho kuwasiliana naye alisema kwamba ni muda mrefu.

Waandishi wa sani walifika kituo kidogo hananasifu na kuonana na mkuu wa kituo hicho aliye fahamika kwa jina moja la chalo, alipoulizwa kama alisikia taarifa za unyama alidai kwamba yeye si msemaji.

Habari kwa hisani ya Gazeti la Sani toleo namba 860

KUCHAKACHUA KUMEHAMIA KWA WAENDESHA MAGUTA TOKA KWA MADRREVA WA MAGARI YA MAFUTA


Pichani ni madreva wa guta wakichakachua mzigo wa ndizi kama walivyo kutwa na kamela yetu.

Kutokana na ugumu wa maisha unaoendelea kuwakabili watanzania sasa waendesha maguta wamekuja na mbinu ya aina yake ya kukabiliana na ugumu wa maisha. wakipewa mzigo toka sokoni kupeleka sehemu yeyote kwanza wanapitia kwenye maskani yao wanachakachua alafu ndo wanaupeleka mzigo kwa muhusika.

KIVUKO CHA MV KIGAMBONI ASUBUHI YA LEO

Tuesday, November 15, 2011

HABARI NJEMA KWA WATANZANIA WALIO PATA AJALI ZA KUVUNJIKA



Blog ya Ustawi blog imepata habari nzuri toka kwa wasamalia wema za kuwepo mtu anaye tibia watu walio pata ajali na kuvunjika. baada ya kupata habari hizo Ustawi blog tumeenda kumtembelea mtaalamu huyo anaye tibia kwa kutumia mitishamba na kudhibitisha juu ya tulicho kisikia. Tumefanya mahojiano na watu zaidi ya 50 walio pata tiba toka kwake na wengine wanaoendelea kupata tiba wametudhihirishia hilo. Mbali na hapo miongoni mwa watu hao wamo viongozi mbalimbali wa serikali ambao nao wamepata tiba toka kwake. hivyo basi kama unandugu yako yeyote amevunjiaka ama unataka kujiridhisha juu ya haya tuyasemayo wasiliana nasi kwa namba 0715 484866 nasi tutakupeleka moja kwa moja hadi kwake.

SERIKALI IMEWACHOKA WALALA HOI

Muswada wa Katiba Mpya: Hotuba ya Msemaji wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (Tundu Lissu)


Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
Mh. Tundu Lissu.
MAONI YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, WIZARA YA KATIBA NA SHERIA, MHESHIMIWA TUNDU A.M. LISSU (MB.)KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA, 2011
(Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, 2007)

UTANGULIZI


Mheshimiwa Spika,
Tarehe 11 Machi 2011, Serikali ilichapisha Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 katika Gazeti la Serikali la tarehe hiyo.

Muswada huo ulipelekwa katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Hati ya Dharura. Hata hivyo, baada ya upinzani mkubwa dhidi ya Muswada huo kujitokeza karibu nchi nzima, Bunge lililazimika kuondoa Hati ya Dharura na hivyo kufanya Muswada kushughulikiwa kwa mujibu wa utaratibu wa kawaida wa kutunga sheria uliowekwa na kanuni za 80, 83 na 84 za Kanuni za Kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano, 2007. Katika kufanya hivyo, Bunge – kwa kupitia Spika - liliiagiza Serikali kufanya mambo yafuatayo kwa mujibu wa Taarifa Rasmi ya Majadiliano Katika Bunge (Hansard) ya Kikao cha Nane cha Mkutano wa Tatu cha tarehe 15 Aprili 2011:


(a) “Muda zaidi utolewe kwa Kamati na wananchi kuufikiria Muswada huu. Katika kufanikisha hili, “... iandae Muswada huu kwa lugha ya Kiswahili ili wananchi wenyewe waweze kusoma yaliyomo kwenye Muswada huo badala ya kupewa tafsiri tu na watu wengine;


(b) “Muswada uchapishwe kwenye magazeti na kutangazwa kwenye vyombo mbali mbali vya habari ili kutoa fursa ya kutosha kwa wananchi wengi kuuelewa na kuutolea maoni;

(c) “Utangulizi wa Muswada huu uwekwe vizuri zaidi ili wananchi waelewe madhumuni ya Muswada huu, kwani imeonekana wazi wananchi wengi wanadhani tayari tumeanza kuandika Katiba, kumbe lengo la Muswada huu ni kutunga Sheria ya Kuunda Tume ya Kukusanya Maoni tu.” (uk. 31-32)

Mheshimiwa Spika,
Katika kutoa maagizo haya, Bunge lilisitiza kwamba “... Muswada huu uko ndani ya Bunge, hauko serikalini.” (uk. 33) Hii ni kwa sababu, kwa mujibu wa kanuni ya 84(1) ya Kanuni za Bunge,Muswada ulikwishasomwa kwa mara ya kwanza na kupelekwa kwenye Kamati inayohusika kwa ajili ya kuanza kujadiliwa.

Aidha, kwa mujibu wa kanuni ya 84(2) Kamati ilikwishaanza kupokea maoni ya wadau “... kwa lengo la kuisaidia katika uchambuzi wa Muswada huo.” Kazi iliyokuwa imebaki kwa Kamati ilikuwa ni kutumia mamlaka yake chini ya kanuni ya 84(3) “... kufanya marekebisho katika Muswada wa Sheria kwa kumshauri Waziri ... anayehusika na Muswada huo kufanya mabadiliko....” Ni baada tu ya kupata ushauri wa Kamati kuhusu mabadiliko ndio Serikali ingeweza kuleta Jedwali la Mabadiliko kwa lengo la kufanya mabadiliko katika hatua hii kabla Muswada haujaletwa Bungeni kwa ajili ya kusomwa mara ya pili na kwa mjadala wa Bunge zima.

Mheshimiwa Spika,
Hakuna hata moja ya maagizo haya ya Bunge ambalo limetekelezwa na Serikali. Tafsiri ya Kiswahili ambayo imeletwa Bungeni – pamoja na kuonyesha imesainiwa tarehe 8 Machi 2011 sawa na Muswada wa Zamani uliopigiwa kelele sana na wananchi – ililetwa kwenye Kamati wiki mbili zilizopita, ikiwa ni wiki moja baada ya Kamati kukataa kuujadili Muswada Mpya kwa vile ulifanyiwa mabadiliko na Serikali bila kupata ushauri wa Kamati kama inavyotakiwa na kanuni ya 83(4) ya Kanuni za Bunge. Badala ya kutekeleza maagizo ya Bunge, Serikali imeleta Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 ambao ulichapishwa katika Gazeti la Serikali la tarehe 14 Oktoba 2011.

Muswada huu mpya una tofauti kubwa na za kimsingi na Muswada wa Zamani kama nitakavyoonyesha hapa. Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, mabadiliko makubwa na ya kimsingi yaliyofanywa kwenye Muswada wa Zamani yalihitaji na bado yanahitaji mjadala wa kitaifa wa wananchi kama ambavyo wengi wamedai katika mijadala inayoendelea nchi nzima.

Aidha, Bunge hili tukufu lilihitaji, na bado linahitaji, muda zaidi wa kuyatafakari mabadiliko haya makubwa nay a kimsingi katika Muswada wa Zamani. Katika mazingira haya, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini ni busara na ni sound policy kwa Muswada huu Mpya kusomwa mara ya Kwanza ili kuruhusu mjadala unaohitajika kufanyika.

TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

Mheshimiwa Spika,
Kama ilivyokuwa kwa Muswada wa Zamani, Muswada huu unapendekeza kuundwa kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo, kwa mujibu wa Utangulizi wa Muswada, itawajibika “... kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi juu ya Katiba (na) kuainisha na kuchambua maoni ya wananchi....” Kwa mujibu wa ibara ya 5, Tume hii itaundwa na Rais “kwa kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar, na kwa ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar....” Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 6(1), Rais atateua wajumbe wa Tume “... kwa kushauriana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar....”

Ibara ya 6(2) inapendekeza kwamba “... muundo wa Tume utazingatia msingi wa kuwepo kwa uwakilishi ulio sawa kwa kila upande wa Jamhuri ya Muungano.” Pendekezo hili linarudia, kwa njia iliyojificha zaidi,msimamo wa ibara ya 6(2) ya Muswada wa Zamani iliyokuwa imeweka wazi kwamba idadi ya wajumbe wa Tume itakuwa sawa kwa sawa kwa pande zote za Jamhuri ya Muungano!

Kama ilivyokuwa kwa Muswada wa Zamani, ibara ya 7(2) ya Muswada inapendekeza kwamba “uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti utafanyika kwa msingi kwamba iwapo Mwenyekiti atatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Makamu Mwenyekiti atakuwa mtu anayetoka upande mwingine wa Jamhuri ya Muungano.”

Muundo wa Tume unakamilishwa na Sekretarieti ya Tume itakayoongozwa na Katibu. (ibara ya 13(1) Kwa mujibu wa ibara ya 13(2), Katibu huyo atateuliwa na Rais “baada ya kukubaliana na Rais wa Zanzibar.” Watendaji wengine wa Sekretarieti watateuliwa na Waziri “kwa makubaliano na Waziri mwenye dhamana ya mambo ya Katiba wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.”

Muswada unapendekeza kumpa Rais - baada ya makubaliano na Rais wa Zanzibar - mamlaka ya kutoa hadidu za rejea za Tume na muda wa kukamilisha na kuwasilisha ripoti. (ibara ya 8(1) Na kama hali itahitaji kufanya hivyo, Rais – “kwa makubaliano na Rais wa Zanzibar” – anaweza kuongeza muda usiozidi miezi mitatu ili kuwezesha Tume kukamilisha na kuwasilisha ripoti. (ibara ya 8(2) Hadidu za rejea, kwa mujibu wa ibara ya 8(3), “... zitakuwa ni hati ya kisheria ambayo Tume itaizingatia katika utekelezaji wa majukumu na utumiaji wa mamlaka yake kwa mujibu wa Sheria hii.”

Mheshimiwa Spika,
Ibara ya 9(1) ya Muswada inaelezea kazi za Tume kuwa ni pamoja na:
(a) Kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi;
(b) Kupitia na kutafiti usahihi na ulinganifu wa masharti ya kikatiba yanayohusu mamlaka ya watu, mifumo ya kisiasa, demokrasia, utawala wa sheria na utawala bora;
(c) Kutoa mapendekezo kwa kila hadidu ya rejea; na
(d) Kuandaa na kuwasilisha ripoti.

Ijapokuwa haijaanishwa hivyo, ni wazi - kwa mujibu wa wa ibara ya 17(1)(d) na (2) ya Muswada - kwamba moja ya kazi za Tume ni kuandaa Rasimu ya Muswada wa Katiba mpya. Mapendekezo ya Muswada kuhusu Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni muhimu na yanazua maswali mengi yanayohitaji mjadala wa kitaifa na maamuzi ya wananchi. Maeneo haya muhimu ni pamoja na nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano katika mchakato mzima wa kutengeneza Katiba Mpya.

MAMLAKA YA RAIS

Mheshimiwa Spika,
Kama ambavyo tumepata kusema ndani ya Bunge hili, kwa muda wote wa uhai wetu kama taifa huru, mfumo wetu wa kikatiba na wa kisiasa umejengwa juu ya nguzo kuu ya Urais wa Kifalme (Imperial Presidency). Hii inatokana na ukweli kwamba katika mfumo huu, Rais ana madaraka makubwa sana ya kiutendaji na ya kiutungaji sheria.

Vile vile Rais ana kivuli kirefu cha kikatiba juu ya mahakama kwa kutumia mamlaka makubwa aliyonayo katika uteuzi wa viongozi wote wa ngazi za juu za Mahakama. Urais wa Kifalme ndio chanzo kikuu cha kukosekana kwa uwajibikaji katika ngazi zote za serikali na ndio kichocheo kikubwa cha rushwa na ufisadi wa kutisha ambao umefanywa kuwa ni sehemu ya kawaida ya maamuzi ya kiserikali.

Sio vibaya, katika kuthibitisha jambo hili, kurudia maneno ya ibara ya 37(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977: “... Rais atakuwa huru na hatalazimika kufuata ushauri atakaopewa na mtu yeyote....” Na kama alivyowahi kusema Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwenye mahojiano ya mwaka 1978 na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), kama Rais wa Tanzania alikuwa na mamlaka – kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi yetu – ya kuwa dikteta!

Muswada unaendeleza kivuli kirefu cha Urais wa Kifalme katika mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya. Mtu mwenye mamlaka ya kidikteta, kama Rais alivyo kwa mujibu wa Katiba ya sasa, hawezi kusimamia upatikanaji wa katiba ya kidemokrasia.

Kwa kutumia mamlaka makubwa ya uteuzi wa Tume yanayopendekezwa na Muswada huu, ni wazi Rais Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama tawala cha CCM, atateua wajumbe anaowataka yeye na Rais Ali Mohamed Shein, Makamu wake na pia Rais wa Zanzibar! Ni wazi vile vile kwamba watu watakaoteuliwa na Marais hawa ni watu wasiokuwa tishio kwa status quo kwa maana ya kupendekeza mabadiliko makubwa katika mfumo wa kikatiba na kiutawala na hivyo kuhatarisha maslahi ya CCM!

Mheshimiwa Spika,
Hali ni hiyo hiyo kwa Sekretarieti ya Tume ambayo ndio chombo cha kiutendaji na moyo wa Tume yenyewe. Kama Katibu, ambaye ndiye mtendaji mkuu wa Tume ni mteuliwa wa Rais na ni mtumishi wa Serikali; kama watendaji wengine wa Tume ni watumishi wa serikali walioteuliwa wa Waziri ambaye naye ni mteuliwa wa Rais baada ya kukubaliana na Waziri mwenzake wa Zanzibar; na kama watumishi wengine wa Tume nao ni watumishi wa Serikali kama inavyopendekezwa na ibara ya 13 ya Muswada Mpya, ni wazi, kwa hiyo, kwamba mapendekezo haya yote ya uteuzi wa wajumbe, watendaji na watumishi wengine wa Tume yana lengo moja tu: kuhakikisha kwamba matokeo ya kazi ya Tume hiyo ni yale tu yanayotakiwa na Rais na Serikali yake na chama chake cha CCM.

Mheshimiwa Spika,
Badala ya mapendekezo haya ya Muswada Mpya, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza utaratibu wa kidemokrasia zaidi katika uteuzi wa Tume. Kwanza, badala ya Tume hiyo kuwa ‘Tume ya Rais’ kama inavyopendekezwa katika Muswada, tunapendekeza iwe ‘Tume ya Vyama’ (multiparty Commission) kwa maana moja kubwa: wajumbe wa Tume wateuliwe kufuatana na mapendekezo na makubaliano ya vyama vya siasa vyenye uwakilishi Bungeni, vyama vingine vilivyosajiliwa pamoja na mashirika ya kijamii, taasisi za kitaaluma na za kidini.

Hii haina maana kwamba wajumbe wa Tume hiyo hawatatakiwa kuwa na sifa zilizoainishwa katika ibara ya 6(3) ya Muswada Mpya. La hasha! Wajumbe wa Tume ya Vyama watatakiwa kuwa na sifa zozote za kitaaluma zinazotakiwa ili kuwawezesha kufanya kazi ya kitaalamu kama inavyopendekezwa na Muswada Mpya.

Pili, baada ya uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Vyama, inapendekezwa kwamba wajumbe walioteuliwa kwa mashauriano na makubaliano kama tunavyopendekeza watatakiwa wathibitishwe na Bunge la Jamhuri ya Muungano. Pendekezo hili litahakikisha kwamba wajumbe wa Tume wanakuwa vetted na chombo kikuu cha uwakilishi wa wananchi. Hili litajenga kuaminiana baina ya Serikali, vyama vya siasa, mashirika ya kijamii, taasisi za kitaaluma na za kidini na litaipa Tume ya Mabadiliko ya Katiba uhalali mkubwa wa kisiasa, kitu ambacho ni muhimu katika mazingira ya sasa ya kisiasa.

Mheshimiwa Spika,
Tofauti pekee na muhimu kati ya pendekezo la Muswada Mpya na pendekezo letu kuhusu mamlaka ya uteuzi wa wajumbe wa Tume ni locus ya uwajibikaji wao. Wajumbe wanaoteuliwa na Rais wanakuwa na shinikizo la kutoa matokeo yatakayompendezesha Rais au chama chake.

Wajumbe wanaotokana na mapendekezo na makubaliano ya wadau wengi na wanaothibitishwa na chombo cha uwakilishi cha wananchi kama tunavyopendekeza hawawezi kuwa na shinikizo la kutoa matokeo yatakayompendezesha mmojawapo wa wadau hao. Faida kubwa na ya wazi ya Tume ya Vyama ni kwamba matokeo ya kazi yake yana nafasi kubwa zaidi ya kukubaliwa, kuheshimiwa na kutekelezwa na wadau mbali mbali kuliko matokeo ya kazi ya Tume ya Rais. Kwa lugha nyingine, kazi ya Tume ya Vyama itakuwa na uhalali wa kisiasa (political legitimacy) mkubwa zaidi kuliko Tume ya Rais.

Pendekezo hili linawahusu Katibu, watendaji na watumishi wengine wa Tume vile vile. Kutokana na uzoefu uliotokana na historia yetu na mfumo wetu wa kiutawala na kikatiba, watumishi wa serikali wamekuwa hawana uhuru wa kufanya maamuzi kwa kuzingatia utashi wao na uadilifu wa kitaaluma bali hufanya maamuzi kwa kuzingatia matakwa ya mabosi wao wa kisiasa.

Hii ni kwa sababu, kisheria na hata kivitendo, watendaji na watumishi karibu wote wa umma hujiona wanawajibika kwa mamlaka zao za uteuzi, yaani Rais na/au Waziri. Aidha, watendaji na watumishi hawa wanawajibika kinidhamu kwa mamlaka zinazoongozwa na watendaji wa Serikali ambao nao ni wateuliwa wa Rais na kwa hiyo wanakuwa na woga wa kufanya maamuzi yanayoweza kuhatarisha maslahi ya kisiasa ya Rais na chama tawala.

Kwa sababu hizo, ni muhimu kwa watendaji na watumishi wote wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wawe huru dhidi ya mashinikizo yoyote ya kisiasa kutoka kwa Rais na Serikali yake na chama chake. Ili Tume iwe na mamlaka na uhuru unaohitajika kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake na ili isiingiliwe kweli na mtu au mamlaka yoyote kama inavyosema ibara ya 10 ya Muswada, inabidi mamlaka ya uteuzi yaondolewe katika mikono ya Rais na/au Waziri ambaye ni mdau mmojawapo tu wa wadau wengi wa mchakato wa Katiba Mpya.

Na namna ya pili ya kuhakikisha uhuru huu unakuwepo ni kuweka utaratibu wa kuwapata watendaji na watumishi hawa nje kabisa ya utumishi wa serikali kwa kuweka masharti ya kuwataka waombe kazi, kufanyiwa usaili na kuteuliwa na jopo la wataalamu walio huru.

Mheshimiwa Spika,
Namna ya tatu ya kuhakikisha uhuru wa Tume katika kutekeleza majukumu yake ni kuhakikisha wajumbe wake wanapatiwa ulinzi wa ajira zao (security of tenure) sawa na wanaopatiwa majaji wa Mahakama ya Tanzania ili kuzuia uwezekano wa wajumbe kuondolewa kwa sababu zisizotokana na utendaji wao wa kitaaluma au ukosefu wa maadili.

Kwa maana hiyo, mapendekezo ya ibara ya 10 Muswada Mpya juu ya uhuru wa Tume hayatoshelezi hata kidogo. Hii ni kwa sababu ibara ya 12 ya Muswada Mpya, ambayo inazungumzia ukomo wa ujumbe wa Tume, haijaweka utaratibu wowote wa namna ya kushughulikia nidhamu ya wajumbe pale kunapokuwepo tuhuma za ukiukaji wa Kanuni za Maadili zinazopendekezwa katika ibara ya 12(2) na Jedwali la Pili la Muswada.

Kutokuweka utaratibu huu kuna hatari kubwa kwani, kisheria, mamlaka ya uteuzi huwa ndio mamlaka ya nidhamu pale ambapo sheria haijaweka utaratibu tofauti wa nidhamu. Hii ina maana kwamba bila kuweka utaratibu wa kisheria wa nidhamu ya wajumbe wa Tume, Rais ndiye atakuwa na uwezo wa kuwaondoa madarakani kwa sababu yeye ndiye aliyewateua!

Mheshimiwa Spika,
Pendekezo letu la tatu linahusu hadidu za rejea. Hapa kuna hoja za aina mbili. Kwanza, sambamba na pendekezo la kutompa Rais madaraka ya uteuzi wa wajumbe wa Tume, Rais asipewe mamlaka ya kutoa hadidu za rejea kwa Tume.

Pili, kwa vile – kama inavyopendekezwa katika Muswada Mpya – hadidu za rejea ni hati ya kisheria inayotakiwa kuzingatiwa na Tume katika utekelezaji wa majukumu yake, ni muhimu hati hii iwekwe wazi katika sheria yenyewe badala ya kubakia kuwa siri ya Rais.

Watanzania lazima wajue Tume inapewa majukumu gani ya kisheria. Aidha, wajumbe wa Tume wenyewe lazima wafahamu wanapewa majukumu gani ya kisheria na wafahamu kwamba wanatakiwa kufuata matakwa ya sheria na sio maelekezo ya mtu mmoja hata kama ni Rais wa Kifalme. Hii itasaidia uwajibikaji wa Tume kwa wananchi kwani itakuwa rahisi kupima matokeo ya kazi ya Tume kwa hadidu za rejea zilizowekwa wazi katika sheria.

Ukweli ni kwamba badala ya kumsubiri Rais kutoa hadidu za rejea, tayari ibara za 9 na 16 za Muswada Mpya zimeshafanya hivyo kwa kuainisha kazi za Tume, mipaka ya Tume katika utekelezaji wa kazi hizo na utaratibu wa namna ya kuzifanya.

Kwa ajili hiyo, zaidi ya kutaka kuonyesha kwamba Rais ana mamlaka makubwa katika mchakato mzima wa upatikanaji wa Katiba Mpya, mapendekezo ya ibara ya 8 hayana maana wala sababu yoyote na yanaweza kuondolewa bila kuathiri maudhui ya Muswada. Aidha, kwa kuzingatia mapendekezo ya ibara ya 9,haijulikani Rais atatoa maelekezo gani ya ziada yanayohusu kazi za Tume na namna ya kuzitekeleza.

Kwa upande mwingine, mapendekezo ya ibara ya 8 yanaweza kuleta mkanganyiko na mgogoro wa kisiasa na kisheria usiokuwa wa lazima endapo Rais atatoa hadidu za rejea zinazotofautiana na matakwa ya kisheria kama yanavyopendekezwa na ibara 9 ya Muswada Mpya. Pendekezo letu, kwa hiyo, ni kwamba ibara ya 8 ifutwe yote na ibara za 9 na 16 zifafanuliwe vizuri ili kuweka wazi zaidi hadidu za rejea za Tume na namna ya kuzitekeleza.

Mheshimiwa Spika,
Kuna mapendekezo mengine yaliyoko kwenye Muswada yanayoonyesha hatari za Urais wa Kifalme. Kama tulivyoona, Tume inatakiwa kuwasilisha ripoti yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano na kwa Rais wa Zanzibar. Baada ya hapo, kwa mujibu wa ibara ya 18(2) ya Muswada, “baada ya mashauriano na makubaliano na Rais wa Zanzibar na baada ya kumalizika kwa taratibu za ndani zinazohusu utungaji wa sera, Rais atamwelekeza Waziri kuwasilisha Muswada wa Katiba katika Bunge la Katiba kwa ajili ya kupitishwa kwa vifungu vya Katiba.”

Pendekezo hili ni la hatari kubwa. Kwanza, ‘kumalizika kwa taratibu za ndani zinazohusu utungaji wa sera’ maana yake ni baada ya kukamilika kwa utaratibu wa kawaida wa kiserikali unaohusu utungaji sera na sheria. Chini ya utaratibu huu, rasimu ya muswada hupelekwa kwanza kwenye Kamati ya Watalaam ya Baraza la Mawaziri (Inter Ministerial Technical Committee of the Cabinet) kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho na Makatibu Wakuu kabla ya kupelekwa kwenye Baraza la Mawaziri kwa maamuzi ya mwisho. Baada ya maamuzi ya mwisho ya Baraza la Mawaziri, rasimu ya muswada hurudishwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuandikwa upya ndipo upelekwe Bungeni la Katiba.

Katika hatua zote hizi, muswada wa sheria huweza kufanyiwa marekebisho makubwa. Kwa maana hiyo, pendekezo la kuuwasilisha Muswada wa Katiba Mpya katika Bunge la Katiba baada ya kuupitisha kwanza kwa Makatibu Wakuu ambao wote ni wateuliwa wa Rais, na kwenye Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe wake wote (ukiacha Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar) ni wateuliwa wa Rais ni kutengeneza mazingira ya kisheria yatakayoruhusu uchakachuaji wa Muswada huo kwa lengo la kuhakikisha matokeo yake ya mwisho, yaani Katiba Mpya, yanakidhi maslahi ya Rais na chama chake cha CCM. Kwa vyovyote vile, pendekezo hili halikubaliki kwa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

SIFA ZA WAJUMBE

Mheshimiwa Spika,
Muswada Mpya unapendekeza sifa zifuatazo wanazotakiwa kuwa nazo wajumbe wa Tume:
(a) Uzoefu katika kufanya mapitio ya katiba na sifa za kitaaluma za wajumbe kwenye mambo ya katiba, sheria, utawala, uchumi, fedha na sayansi ya jamii;
(b) Jiografia na mtawanyiko wa watu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(c) Maslahi ya umma;
(d) Umri, jinsia na uwakilishi wa makundi mbali mbali ya kijamii; na
(e) Vigezo vingine ambavyo Rais ataona vinafaa. (ibara ya 6(3)
Zaidi ya sifa zilizotajwa, ibara ya 6(4) inakataza watu wenye sifa zifuatazo kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume:
(a) Wabunge, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, madiwani na viongozi wa vyama vya siasa wa ngazi zote kuanzia Wilaya hadi Taifa;
(b) Watumishi wa vyombo vya usalama;
(c) Watu waliowahi kuhukumiwa kwa kutenda kosa au wanaotuhumiwa mahakamani kwa mashtaka ya kukosa uaminifu au uadilifu;
(d) Watu wasiokuwa raia wa Tanzania.

Mapendekezo haya yana athari kubwa kwa mchakato mzima wa upatikanaji wa Katiba Mpya. Kwanza, kwa kukataza viongozi wa ngazi za juu na za kati wa vyama vya siasa kuteuliwa wajumbe wa Tume kunaondoa kwenye mchakato wa Katiba Mpya kundi kubwa la watu wenye utaalamu na uzoefu katika masuala mbali mbali ya kisiasa, kikatiba, kisheria, kiuchumi, kiutawala, kifedha na kisayansi jamii.

Vile vile, viongozi wa vyama vya siasa wanawakilisha makundi makubwa ya kijamii yenye mtawanyiko wa watu na wa kijiografia katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na wanawakilisha watu wa umri na jinsia zote kama inavyopendekezwa katika Muswada Mpya.

Aidha, kwa kuwa maneno ‘maslahi ya umma’ hayajafafanuliwa katika Muswada, hakuna anayeweza kudai kwamba viongozi wa ngazi za juu na za kati wa vyama vya siasa vilivyosajiliwa kisheria baada ya kutimiza masharti yote husika ya kisheria, na ambao wanaungwa mkono na mamilioni ya wananchi wa Tanzania kwa kupewa nafasi za uwakilishi katika taasisi za uwakilishi za umma kama Bunge, Baraza la Wawakilishi na Halmashauri za Serikali za Mitaa hawajui wala hawazingatii maslahi ya umma na kwa hiyo hawafai kuwakilishwa katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba!

Kama ingekuwa hivyo, Rais – ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM na kwa hiyo kiongozi wa chama cha siasa – naye pia atakuwa hana sifa za kuteua Tume! Na wakati haja ya kutoshirikisha watumishi wa taasisi za ulinzi na usalama katika mchakato wenye ubishani wa kisiasa kama utungaji wa Katiba Mpya inaeleweka, ni matusi kwa watu waliochaguliwa na wananchi kuwa Wabunge, Wawakilishi au Madiwani au viongozi wa vyama vya siasa vilivyowapendekeza watu hao, kuwekwa pamoja na wahalifu na kutamkwa kuwa hawana sifa za kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba!

Inaelekea lengo kuu la pendekezo hili ni kuhakikisha kwamba vyama vya upinzani, hasa hasa CHADEMA, vyenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya Bunge havipati fursa ya kuamua muundo na maudhui ya Katiba Mpya hasa katika hatua muhimu za uundaji wake. Pili, lengo kuu vile vile ni kuhakikisha kuwa Rais, na kwa hiyo chama chake cha CCM, wanadhibiti mchakato wa Katiba Mpya katika hatua muhimu ya uundaji wake.

Endapo watafanikiwa katika hili, Rais na chama chake cha CCM watakuwa na nafasi kubwa ya kuamua aina ya Katiba Mpya itakayotokana na mchakato walioudhibiti kama inavyopendekezwa na Muswada Mpya. Hii ni kwa sababu, kwa kutumia uzoefu wa Tume nyingine zilizopata kuteuliwa miaka ya nyuma, wajumbe wengi huwa ni watumishi au waliopata kuwa watumishi wa Serikali na/au taasisi zake. Wajumbe wa aina hii wamekuwa hawana uthubutu wa kupendekeza mabadiliko makubwa yanayohitajika katika mfumo wa utawala wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika,
Badala ya kukataza viongozi wa vyama vya siasa kama inavyopendekezwa na Muswada Mpya, na kwa kuzingatia nafasi ya vyama vya siasa katika historia yetu na mfumo wetu wa utawala, na kwa lengo la kuhakikisha Tume inakuwa na utaalamu, uzoefu na uhalali wa kisiasa unaohitajika, watu wanaostahili kuteuliwa kuwa wajumbe wa Tume wawe ni wale wenye sifa zinazopendekezwa na ibara ya 6(3)(a), (b), (c) na (d) ya Muswada.

Kwa sababu hiyo, hakutakiwi kuwa na vigezo vingine visivyojulikana wazi kwa wananchi. Kwa maneno mengine, pendekezo la kuwa na ‘vigezo vingine ambavyo Rais ataona inafaa’ halikubaliki kwani linampa Rais mwanya wa kuteua marafiki zake au watu ambao hawana sifa zinazojulikana. Kwa maoni yetu vile vile, badala ya kuwa sababu ya disqualification, uongozi wa kuchaguliwa na wananchi katika taasisi za uwakilishi au katika vyama vya siasa unatakiwa kuwa an added advantage pale ambapo kiongozi husika ana sifa za kitaaluma zinazotakiwa!

MISINGI MIKUU YA KITAIFA

Mheshimiwa Spika,
Muswada unapendekeza kuwepo kwa ‘misingi mikuu ya kitaifa’ ambayo Tume inatakiwa kuizingatia kwa lengo la kuihifadhi na kuidumisha. Misingi mikuu inayopendekezwa ni:
(a) Kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano;
(b) Uwepo wa Serikali, Bunge na Mahakama;
(c) Mfumo wa kiutawala wa kijamhuri;
(d) Umoja wa kitaifa, amani na utulivu;
(e) Uchaguzi wa kidemokrasia wa mara kwa mara katika vipindi maalum kwa kuzingatia haki ya watu wote kupiga kura;
(f) Ukuzaji na na uhifadhi wa haki za binadamu;
(g) Utu, usawa mbele ya Sheria na mwenendo wa sheria; na
(h) Uhuru wa kuabudu na uvumilivu wa dini nyingine. (ibara ya 9(2)

Kifungu hiki kimefanyiwa mabadiliko kwa kufuta maneno ‘Tume itahakikisha ... kutokugusika na utakatifu (inviolability and sanctity) wa mambo yafuatayo’ yaliyokuwa katika Muswada wa Zamani, na badala yake yamewekwa maneno mapya ‘... kuhifadhi na kudumisha mambo yafuatayo....’ Mabadiliko haya yamefanywa ili kujaribu kuondoa hofu iliyojitokeza wakati wa mikutano ya kukusanya maoni ya wadau kwamba lengo la pendekezo hilo lilikuwa kuzuia mjadala juu ya masuala ya kikatiba yenye utata mkubwa kama vile suala la Muungano.

Hata hivyo, hatari ya kuzuiliwa kwa mjadala juu ya misingi mikuu ya kitaifa bado haijaondolewa kwani, kwa mujibu wa ibara mpya ya 9(3), “... Tume itatoa fursa kwa watu kutoa maoni yao kwa uhuru kwa lengo la kuendeleza na kuboresha masuala hayo.” Tafsiri halisi ya maneno haya ni kwamba mjadala pekee utakaoruhusiwa juu ya ‘misingi mikuu ya kitaifa’ ni ule ambao lengo lake ni ‘kuendeleza na kuboresha masuala hayo.’

Kwa maoni yetu, lengo kuu la pendekezo linalohusu kuendeleza na kuboresha ‘misingi mikuu ya kitaifa’ ni kuzuia mjadala wenye kuhoji ‘kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano’ ili kuendeleza mfumo wa sasa wa Muungano wenye Serikali mbili. Hii ni kwa sababu katika mambo yote yanayopendekezwa kuwa misingi mikuu ya kitaifa, ni ‘kuwepo kwa Jamhuri ya Muungano’ yenye Serikali mbili ndio ambayo imekuwa na mgogoro mkubwa kwa muda wote wa maisha ya Jamhuri ya Muungano.

Ukiacha ‘ukuzaji na uhifadhi wa haki za binadamu’ ambalo lilikataliwa na Serikali ya Mwalimu Nyerere kwa miaka yote ya utawala wake, mambo mengine yote yanayotajwa kuwa ‘misingi mikuu ya kitaifa’ hayajawahi kubishaniwa kwa miaka yote ya uhai wa Jamhuri ya Muungano.

Mheshimiwa Spika,
Pendekezo la ‘misingi mikuu ya kitaifa’ linastaajabisha sana kwani, kwa mujibu wa ibara ya 98(1)(b) ya Katiba ya sasa, ‘kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano, Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, madaraka ya Serikali ya Kamhuri ya Muungano, kuwapo kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano, madaraka ya Serikali ya Zanzibar, Orodha ya Mambo ya Muungano na idadi ya Wabunge kutoka Zanzibar’ ni mambo yanayoweza kubadilishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ili mradi tu mabadiliko hayo yaungwe mkono na theluthi mbili ya Wabunge wote wa kutoka Tanzania Bara na wa Tanzania Zanzibar.

Kwa sababu hiyo, pendekezo la ibara ya 9(3) ya Muswada kwamba ‘misingi mikuu ya kitaifa’ izungumzwe kwa lengo la kuiendeleza na kuidumisha tu halikubaliki kwa sababu linazuia uhuru wa kuhoji na/au kupinga mambo ambayo kwa Katiba ya sasa ni ruhusa kuyahoji, kuyapinga na/au hata kuyabadilisha! Tunapendekeza ibara ya 9(2) na (3) za Muswada zifutwe kabisa ili kuwepo na uhuru kamili wa kujadili, kwa kupinga au kuunga mkono, kila jambo linalohusika na Katiba Mpya.

NAFASI YA ZANZIBAR

Mheshimiwa Spika,
Pengine mabadiliko makubwa yaliyofanywa katika Muswada ni mapendekezo yanayohusu nafasi ya Zanzibar katika mchakato wa Katiba Mpya. Itakumbukwa kwamba moja ya masuala yaliyozua tafrani kubwa katika mchakato wa kukusanya maoni juu ya Muswada wa Zamani hasa katika kituo cha Zanzibar ni kuwepo hisia kwamba nafasi ya Zanzibar ilikuwa imepuuzwa katika Muswada huo.

Muswada sio tu kwamba umetekeleza matakwa yote ya ushirikishwaji wa Zanzibar, bali umekwenda mbali zaidi kwa kuifanya Zanzibar mwamuzi wa mustakbala wote wa kikatiba wa Tanzania. Hii imefanyika kwa njia mbili: kwanza, kwa kumfanya Rais wa Zanzibar kuwa mshirika sawa wa kikatiba wa Rais wa Jamhuri ya Muungano; na pili, kwa kuipa Zanzibar nafasi kubwa ya uwakilishi katika mchakato mzima wa Katiba Mpya.

NAFASI YA RAIS WA ZANZIBAR

Mheshimiwa Spika,
Muswada unapendekeza kwamba utekelezaji wa mamlaka yote ya Rais, Waziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano lazima ufanyike kwa ‘mashauriano na makubaliano’ na Rais, Waziri au Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar.

Kwa mfano, ibara ya 5 inayohusu kuundwa kwa Tume inamtaka Rais ‘kushauriana na kukubaliana’ na Rais wa Zanzibar na kupata ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar. Vile vile, ibara ya 6(1) inayohusu uteuzi wa wajumbe wa Tume; ibara ya 8(1) na (2) inayohusu hadidu za rejea na kuongeza muda wa Tume; na ibara ya 13(2) inayohusu uteuzi wa Katibu wa Tume, zote zinataka kuwepo na makubaliano na Rais wa Zanzibar. Aidha, ibara ya 13(5) inayohusu uteuzi wa watendaji wengine wa Tume inalazimu makubaliano kati ya Waziri na Waziri mwenzake wa Zanzibar ambao nao ni wateuliwa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Zanzibar.

Mamlaka ya Rais wa Zanzibar hayaishii tu kwenye uteuzi wa wajumbe na watendaji wa Tume, bali pia yanaingia hata katika uwasilishaji wa ripoti ya Tume. Kwa mujibu wa ibara 18(1) ya Muswada, mara baada ya kumaliza kazi yake, Tume itawasilisha ripoti yake kwa Rais na kwa Rais wa Zanzibar.

Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 18(2), mara baada ya kupokea ripoti hiyo, Rais, ‘baada ya kushauriana na kukubaliana’ na Rais wa Zanzibar, “... atamuagiza Waziri kuwasilisha Muswada wa Katiba katika Bunge la Katiba.” Kwa mapendekezo haya pia, Rais wa Zanzibar sio tu kwamba ana mamlaka karibu sawa na Rais wa Jamhuri ya Muungano bali pia ana kura ya turufu katika mchakato wa Katiba Mpya.

Maana yake ni kwamba Rais wa Zanzibar asipopatiwa nakala ya ripoti ya Tume au asipokubaliana na Rais wa Muungano, basi Muswada wa Katiba hautawasilishwa kwenye Bunge la Katiba!

Mheshimiwa Spika,
Mapendekezo haya yanaashiria kuwepo kwa mtazamo ambao chanzo chake ni Makubaliano ya Muungano kati ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika ya tarehe 25 Aprili 1964. Kwa mtazamo huo, Zanzibar ni nchi huru kama ilivyokuwa mwaka 1964 na kwa hiyo ni lazima sio tu ishirikishwe kwa usawa, bali pia lazima ikubaliane na mabadiliko yoyote ya kikatiba yanayopendekezwa na Muswada.

Kama Profesa Palamagamba Kabudi wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alivyosema kwenye Semina ya Wabunge Juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba iliyofanyika tarehe 12 Novemba 2011: ‘Katika kuandika katiba mpya, wabia wa Muungano wanarudi kwa usawa.’

Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, mtazamo huu sio sahihi. Kwanza kabisa, Zanzibar sio nchi huru tena kama ilivyokuwa mwaka 1964, kama ambavyo hakuna tena nchi inayoitwa Tanganyika wala serikali yake. Hii ni kwa sababu tangu kusainiwa kwa Hati za Muungano mwaka 1964, na kwa mujibu wa ibara ya 4(3) ya Katiba ya sasa, masuala yote yanayohusu Muungano kama vile Katiba ya Tanzania yamekasimiwa kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, ambayo pia imekasimiwa mamlaka juu ya masuala ya iliyokuwa Tanganyika.

Masuala haya ya Muungano hayawezi kujadiliwa upya na kwa usawa kati ya nchi hizi mbili kwa vile moja kati ya nchi hizo haipo tena na iliyobaki imepoteza sehemu ya uhuru wake kutokana na Muungano huo! Hii ndio kusema hakuwezi tena kuwa na wabia wa Muungano bila kwanza kuirudisha Tanganyika kama nchi na bila kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yenye uhuru na mamlaka kama iliyokuwa nayo kabla ya Muungano!
Pili, kuna dhana kwamba Rais wa Zanzibar hakushirikishwa katika mchakato wa maandalizi ya Muswada wa Zamani. Dhana hii vile vile ni potofu.

Kwanza, Rais Ali Mohamed Shein mwenyewe ametamka wazi kwa waandishi wa habari kwamba alishiriki katika hatua zote za maamuzi kwenye Baraza la Mapinduzi. Pili, mujibu wa ibara ya 54(1) ya Katiba ya sasa, Rais wa Zanzibar ni mmoja wa wajumbe wa Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kwa hiyo ni mshiriki wa maamuzi yote ya Serikali hiyo.

Kwa maana hiyo, maslahi ya Zanzibar yanawakilishwa ndani ya ‘chombo kikuu cha kumshauri Rais’ katika Jamhuri ya Muungano. (ibara ya 54(3) Hii ni licha ya ukweli kwamba, kwa mlolongo wa madaraka uliopo katika ibara ya 54(2), Rais wa Zanzibar sio mmoja wa wajumbe wanaoweza kuongoza mikutano ya Baraza hilo.

Aidha, ndani ya Baraza la Mawaziri, Zanzibar inawakilishwa pia na Makamu wa Rais ambaye – kwa mujibu wa ibara ya 47(1) ya Katiba ya sasa – “... ndiye Msaidizi Mkuu wa Rais kuhusu mambo yote ya Jamhuri ya Muungano....” Kwa maana hiyo, mapendekezo ya Muswada yanayomfanya Rais wa Zanzibar kuwa sio tu mshiriki sawa lakini pia mwamuzi wa mustakbala wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano yanaenda kinyume sio tu na Katiba ya sasa bali pia na Hati za Muungano wenyewe. Kwa mapendekezo haya, endapo Rais wa Zanzibar hatakubaliana na uteuzi wowote wa wajumbe wa Tume au Katibu wake au watendaji wake wengine, anaweza kusimamisha mchakato mzima wa kikatiba hata kama unahusu masuala ya Tanzania Bara yasiyo ya Muungano!

UWAKILISHI WA ZANZIBAR

Mheshimiwa Spika,
Ushawishi mkubwa wa Zanzibar hauishii katika kura ya turufu aliyo nayo Rais wa Zanzibar pekee yake. Zanzibar ina ushawishi mkubwa vile vile kutokana na nafasi kubwa iliyo nayo katika vyombo vya maamuzi vinavyopendekezwa na Muswada. Kwa mfano, kwa mujibu wa ibara ya 6(2), “... muundo wa Tume utazingatia msingi wa kuwepo kwa uwakilishi ulio sawa kwa kila upande wa Jamhuri ya Muungano.”

Hii ina maana kwamba wajumbe wa Tume na Sekretarieti yake wanatakiwa wawe sawa kwa sawa kati ya Tanzania Bara na Zanzibar. Ikumbukwe kwamba Tume hii inatengeneza Katiba inayohusu masuala ya Muungano, ambayo ni haki kwa Zanzibar kushirikishwa kwa usawa kabisa, na vile vile masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanzania Bara ambayo Zanzibar haina haki ya kushiriki.

BUNGE LA KATIBA
Mheshimiwa Spika, Eneo la pili ambalo Zanzibar ina ushawishi mkubwa kutokana na uwakilishi wake ni katika Bunge la Katiba linalopendekezwa katika Sehemu ya Tano ya Muswada. Kwa mujibu wa ibara ya 20(2), wajumbe wa Bunge la Katiba watakuwa ni wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano; wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar; mawaziri wa katiba na sheria wa Jamhuri ya Muungano na wa Zanzibar; Wanasheria Wakuu wa Jamhuri ya Muungano na wa Zanzibar; na wajumbe mia moja kumi na sita wakaoteuliwa kutoka asasi zisizokuwa za kiserikali, asasi za kidini, vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, taasisi za elimu ya juu na makundi yenye mahitaji maalum katika jamii. Inaelekea kwamba, kwa mujibu wa ibara ya 20(4), wajumbe wasiokuwa wabunge ama wawakilishi nao pia watateuliwa na Rais licha ya kutoka nje ya mfumo wa kiserikali!

Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa ibara ya 66(1)(a) ya Katiba ya sasa ya Muungano, wajumbe wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ni pamoja na wabunge wa majimbo ya uchaguzi. Kwa composition ya sasa ya Bunge, kuna jumla ya majimbo ya uchaguzi 239 ambayo kati yao majimbo ya Zanzibar ni hamsini. Vile vile, kwa mujibu wa ibara ya 66(1)(c) ya Katiba, Baraza la Wawakilishi Zanzibar linawakilishwa na wabunge watano katika Bunge la Jamhuri ya Muungano. Aidha, kama inavyotakiwa na ibara ya 66(1)(b), kuna wabunge wanawake mia moja na mbili wanaojulikana kama ‘wabunge wa viti maalum.’

Kwa mgawanyo wa sasa wa wabunge hawa, idadi ya wanaotoka Zanzibar ni ishirini na tano kwa vyama vyote vyenye uwakilishi bungeni. Na mwisho, kuna wabunge wasiozidi 10 wanaoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa ibara ya 66(1)(e). Hadi sasa, Rais ameshateua wabunge watatu ambao wote ni wa kutoka Zanzibar. Kwa hiyo, katika Bunge la sasa lenye wabunge 353, wabunge wanaowakilisha Zanzibar ni themanini na tatu au karibu 23.5% ya wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Kwa mujibu wa Sehemu ya Kwanza ya Sura ya Tano ya Katiba ya Zanzibar, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ni pamoja na wawakilishi wa majimbo hamsini ya uchaguzi, wawakilishi kumi wa kuteuliwa na Rais wa Zanzibar na wawakilishi ishirini wa viti maalum na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa hiyo, jumla ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa sasa ni themanini na moja. Kwa maana nyingine ni kwamba endapo mapendekezo ya ibara ya 20(1)(b), (c) na (d) ya Muswada yatakubaliwa, idadi ya wajumbe wa Bunge la Katiba wanaotoka Zanzibar itaongezeka hadi kufikia mia moja sitini na nne kati ya wajumbe 545 wa Baraza hilo kwa mujibu wa ibara ya 20(2). Idadi hii ni sawa na 30% ya wajumbe wote wa Bunge la Katiba.

Idadi hiyo ya uwakilishi wa Zanzibar bado haitakidhi matakwa ya Muswada kwani ibara ya 20(3) inapendekeza kwamba “... idadi ya wajumbe wa Baraza la Katiba kutoka Tanzania Zanzibar ... haitapungua theluthi moja ya wajumbe wote wa Bunge la Katiba”! Theluthi moja ya wajumbe wa Bunge la Katiba ni wajumbe 182.

Kwa hiyo ili kukidhi matakwa ya Muswada kuhusu uwakilishi wa Zanzibar, itabidi wajumbe 18 kati ya 116 waliotajwa na ibara ya 20(2)(e) watoke Zanzibar ili kufikisha idadi ya wajumbe 182 ambayo ndio theluthi moja ya wajumbe wote wa Bunge la Katiba.

Mheshimiwa Spika,
Kuna maeneo mengine ya Muswada ambayo pia yanazua maswali mengi juu ya nafasi ya Zanzibar katika mchakato wa Katiba Mpya. Kwa mfano, wakati ibara ya 21(1) inapendekeza kwamba Spika na Naibu Spika wa Bunge la Katiba wachaguliwe kutoka miongoni mwa wajumbe wa Bunge hilo, ibara ya 21(2) inapendekeza kwamba endapo Spika atatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano basi Naibu wake lazima atoke upande mwingine.

Sambamba na pendekezo hili, ibara ya 22(1) inapendekeza Makatibu wa sasa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar watakuwa ndio Katibu na Naibu Katibu wa Bunge la Katiba. Aidha, sawa na ibara ya 21(2), ibara ya 22(2) inapendekeza kwamba endapo Spika atatoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, basi Katibu wa Bunge la Katiba lazima atoke upande mwingine.

Mapendekezo haya yanaonyesha sio tu nafasi na ushawishi mkubwa wa Zanzibar katika mchakato wa Katiba Mpya, bali pia ni mwendelezo wa dhana potofu kwamba Zanzibar ni mshirika sawa wa Jamhuri ya Muungano.

Hii inathibitishwa pia na pendekezo la ibara ya 24(3) ya Muswada inayotaka Katiba Mpya ikubaliwe na theluthi mbili ya wajumbe wa Bunge la Katiba wanaotoka Tanzania Bara na vile vile theluthi mbili ya wajumbe wanaotoka Zanzibar. Ni wazi, kwa hiyo, kwamba iwe ni kwa masuala ya Muungano yanayoihusu Zanzibar pia, au kwa masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanzania Bara ambayo hayaihusu, Zanzibar itakuwa na kura ya turufu kwa mujibu wa mapendekezo ya Muswada huu.

Mheshimiwa Spika, Uwakilishi mkubwa wa Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano umetumika kihistoria kwa lengo la kuwatuliza Wazanzibari wakati Serikali ya Mwalimu Nyerere ilipokuwa inamomonyoa uhuru wa Zanzibar kwa kuongeza orodha ya Mambo ya Muungano kwenye Katiba ya Muungano.

Katika kitabu chake Pan Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika – Zanzibar Union, Profesa Issa Shivji, mwanazuoni mashuhuri wa kikatiba na mwanafunzi wa historia ya Muungano huu amemnukuu aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wakati wa utawala wa hayati Sheikh Abedi Amani Karume, Bw. Wolfgang Dourado akimnukuu Sheikh Karume juu ya nafasi ya Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano: “‘Msiwe na wasi wasi, sisi tuna haki ya kuwakilishwa katika Bunge lao lakini wao hawana haki ya kuwakilishwa katika Baraza letu la Mapinduzi’”!

Mheshimiwa Spika,
Sababu nyingine inatokana na kuongezeka kwa ushawishi na nafasi ya Zanzibar katika siasa za ndani ya CCM, hasa hasa katika zama hizi za vyama vingi na vita za makundi mbali mbali ndani ya chama hicho. Katika mazingira haya, mtu yeyote anayetaka kupitishwa kuwa mgombea urais kwa kupitia CCM anakuwa anahitaji kura za CCM Zanzibar ili kushinda katika kinyang’anyiro hicho.

Kwa kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere mwenyewe katika kitabu chake Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, “sababu moja kubwa iliyofanya viongozi wetu wasitake kuwaudhi ‘Wazanzibari’ ... ni umuhimu wa kura za Zanzibar katika kumteua mwanachama wa CCM kuwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano.

Kwa kiongozi yeyote anayeliona jambo hilo kuwa ni muhimu kupita mengine yote, kuwaudhi ‘Wazanzibari’ ni dhambi ambayo haina budi iepukwe kwa kila njia.” Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hofu hii ya kuwaudhi ‘Wazanzibari’ ndio imepelekea kimya kikuu – ndani ya CCM na ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano - juu ya ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano uliofanywa na Sheria ya Mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar, 2010.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba upendeleo wa Zanzibar unaopendekezwa katika Muswada huu kuhusiana na uwakilishi katika Bunge la Katiba na katika vyombo vingine vya maamuzi juu ya mchakato wa Katiba Mpya sio wa haki na haukubaliki tena. Kwanza, ibara ya 64(2) ya Katiba ya sasa inaweka wazi kwamba Baraza la Wawakilishi Zanzibar lina mamlaka ya kutunga sheria katika Zanzibar ‘... juu ya mambo yote yasiyo mambo ya Muungano....’

Hii pia ndio lugha ya ibara ya 78(1) ya Katiba ya Zanzibar kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka jana. ‘Katiba ya Tanzania’ ni jambo la kwanza katika orodha ya Mambo ya Muungano iliyoko kwenye Nyongeza ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Kwa Muswada Mpya kupendekeza kwamba Baraza la Wawakilishi Zanzibar liwe sehemu ya Bunge la Katiba ni kukiuka wazi wazi matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na ya Katiba ya Zanzibar. Ni ajabu iliyoje kwamba wale wanaojifanya ni machampioni wa Muungano wanaweza kunyamazia ukiukaji huu wa Katiba!

Mheshimiwa Spika,
Thomas Paine, mwandishi maarufu wa Marekani ya wakati wa Mapinduzi ya mwaka 1776, aliwahi kuandika kijitabu alichokiita Common Sensejuu ya uhalali wa Uingereza kutawala Bara la Amerika ya Kaskazini ambako alisema: ‘... [T]here is something very absurd in supposing a continent to be perpetually governed by an island [for] in no instance hath nature made the satellite larger than its primary planet...’! Yaani, ni ujinga kudhani kwamba bara linaweza kutawaliwa milele na kisiwa kwa sababu utaratibu wa asili haujawahi kufanya kitegemezi kuwa kikubwa kuliko sayari yake ya msingi.

Hata kama ni kweli kwamba Tanganyika sio bara kama ilivyokuwa Marekani ya Kaskazini, bado tunakubaliana na Tom Paine kwamba ni ujinga kudhani kwamba Visiwa vya Zanzibar vitaendelea kuwa na maamuzi na ushawishi mkubwa katika masuala yasiyokuwa ya Muungano ya Tanganyika kwa sababu utaratibu wa asili haujawahi kufanya maslahi ya Visiwa hivyo kuwa bora zaidi ya maslahi ya Tanganyika!
Kwa maoni yetu, wakati umefika kwa Muungano kuwekwa kwenye msingi wa usawa na imara zaidi.

Msingi huo unahitaji kurudishwa tena kwa Serikali ya Tanganyika ambayo ndio ilikuwa – pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar – mbia mkuu wa Muungano wa mwaka 1964. Kurudishwa huko kwa Tanganyika kutaiwezesha Zanzibar kujadiliana nayo kwa usawa juu ya masuala yote yanayohusu Muungano.

Haya yote yanawezekana tu endapo Muungano huu utawekwa mbele ya wananchi ili waamue – kwa kura ya maoni - kama wanataka kuendelea nao au la; na kama wanataka kuendelea nao ni muundo gani wa Muungano wanaoutaka.

Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya kurudishwa kwa Tanganyika na Serikali yake sio mapya. Miaka ishirini iliyopita, Tume ya Rais ya Mfumo wa Chama Kimoja au Vyama Vingi vya Siasa (Tume ya Nyalali) ilipendekeza hivyo hivyo. Miaka saba baadae, Tume ya Kukusanya Maoni Juu ya Katiba, White Paper Na. 1 ya 1998(Tume ya Kisanga) nayo ilipendekeza hivyo hivyo.

Kuendelea kupuuza mapendekezo haya wakati Zanzibar inavunja Katiba ya sasa ya Muungano; kuendelea kukaa kimya kwa hofu ya kuwaudhi ‘Wazanzibari’ wakati wao wanajitwalia uhuru wa kujiamulia mambo yao wenyewe huku wakiendelea kushiriki katika maamuzi ya mambo ya Tanganyika yasiyokuwa ya Muungano; kuendeleza kile alichokiita Mwalimu Nyerere falsafa ya ‘changu ni changu, chako ni chetu’ katika mahusiano ya Zanzibar na Tanzania Bara, ni kutulazimisha tuipinge dhana nzima ya Muungano kati ya nchi zetu mbili kitu kinachoweza kupelekea kuvunjika kwa Muungano wenyewe.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni isingependa tufike huko lakini ndoa hii ya kulazimishana haiwezi ikadumu muda mrefu kwa taratibu za aina hii.

UDHOOFISHAJI WA UPINZANI

Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya Muswada juu ya uwakilishi katika Bunge la Katiba yana athari nyingine kubwa katika majadiliano na maamuzi ndani ya Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na Profesa Issa G. Shivji kwa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, endapo mapendekezo ya ibara ya 20(2) ya Muswada yatapitishwa, CCM itakuwa na kati ya wajumbe 350 hadi 400 katika Bunge la Katiba ambalo lina wajumbe 545.

Kwa upande mwingine Chama cha Wananchi (CUF) ambacho kina Wawakilishi 29 katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kitakuwa na wajumbe 65 katika Bunge la Katiba. Kwa maana ya uwakilishi katika Bunge la Katiba, CUF itakuwa ndio chama cha pili kwa nguvu za kisiasa ndani ya Bunge hilo, licha ya kuwa na wabunge wawili tu wa kuchaguliwa kwa upande wa Tanzania Bara na licha ya kupata kura chache sana katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Na kama inavyojulikana, tangu Muafaka wa Kisiasa Zanzibar kati ya CCM na CUF wa mwaka 2010 na kuzaliwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, upinzani wa kisiasa Zanzibar umekufa na kwa upande wa Tanzania Bara, na hasa Bungeni na kwenye chaguzi ndogo kama ule wa Igunga, CUF imekuwa ikishirikiana na CCM kuipinga CHADEMA.

Kwa mapendekezo haya, kambi ya CCM na CUF katika Bunge la Katiba inaweza kufika hata zaidi ya wajumbe 465 katika ya wajumbe 545 wa Bunge hilo! CHADEMA ambayo kwa sasa ndio chama kinachoongoza Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kutokana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, itabakia na Wabunge wake 48 na vyama vya kibunge vilivyobaki, yaani NCCR-Mageuzi, TLP na UDP vitabaki na jumla ya Wabunge sita.

Kwa hiyo, CHADEMA itakuwa chama cha tatu kwa nguvu za kisiasa ndani ya Bunge la Katiba licha ya kuwa ni chama kikuu cha upinzani chenye nguvu na ushawishi mkubwa wa kisiasa nchini!
Kwa maana nyingine, iwe ni kwa makusudi au bila ya kujua au kwa kunuia, athari mojawapo kubwa ya mapendekezo ya Muswada kuhusu uwakilishi katika Bunge la Katiba itakuwa ni kuiongezea nguvu zaidi kambi ya CCM/CUF na kupunguza nguvu na ushawishi wa CHADEMA ambayo ndio chama pekee kinachobeba matarajio na matamanio ya Watanzania wengi wanaotaka mabadiliko ya kimsingi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika nchi yetu.

Haihitaji kuwa na shahada ya uzamivu kujua kwamba Bunge la Katiba lenye uwakilishi wa aina hii litapitisha Katiba Mpya ambayo pengine itatofautiana na Katiba ya sasa kwa jina tu! Na wala haihitaji kisomo kikubwa kujua kwamba Bunge la Katiba la aina hii halitagusa ‘msingi mkuu’ uliobaki wa Jamhuri ya Muungano, yaani Serikali mbili. Hapa pia ni wazi kuwa lengo halisi la mapendekezo haya ni kuhakikisha kwamba mchakato wa Katiba Mpya utazaa matunda yasiyokuwa tofauti sana na ya Katiba ya sasa!

‘UWAKILISHI’ WA BUNGE LA KATIBA

Mheshimiwa Spika,
Sio Bunge hili tukufu la Jamhuri ya Muungano wala Baraza la Wawakilishi Zanzibar lenye mamlaka kikatiba na kisiasa ya kutunga Katiba Mpya ya Tanzania. Hii ni kwa sababu sisi wote tulioko humu ndani tulichaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya sasa na mamlaka yetu yote yako ndani ya kona nne za Katiba hiyo. Kama ni kweli, kama anavyodai Profesa Kabudi, kwamba kitendo cha kutunga Katiba Mpya vile vile ni kitendo cha kuua Katiba ya Zamani, basi sisi Wabunge na Wawakilishi wa Zanzibar hatuna mamlaka ya kuiua Katiba ya sasa kwa sababu sisi wote tulikula kiapo cha kuilinda, kuihifandhi na kuitetea.

Pili, sisi sote ni Wabunge na Wawakilishi wa vyama vya siasa kwa sababu, kwa mujibu wa Katiba ya sasa sheria zote husika, tumechaguliwa kwa sifa kuu ya kuwa wanachama wa, na tuliopendekezwa na, vyama vya siasa.

Kuligeuza Bunge la Jamhuri ya Muungano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuwa Bunge la Katiba ni sawa na kusema kwamba wasiokuwa wanachama wa vyama vya siasa hawana haki ya kushiriki katika kutunga Katiba Mpya kwa sababu ya kuwa na kilema cha kisheria kinachowakataza kuchaguliwa kuwa Wabunge na Wawakilishi! Ibara ya 20(4) ya Katiba ya sasa inatamka wazi kwamba “... ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote....” Sio kosa, kwa hiyo, kwa mamilioni ya Watanzania ambao wameamua kwa hiari zao kutokuwa wanachama wa vyama vya siasa.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haikubaliani, na haiwezi kukubali, ubaguzi wa aina hii dhidi ya Watanzania walioamua kutumia haki zao za kikatiba ya kutokujiunga na chama chochote cha siasa. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haitakubali Watanzania hao waadhibiwe kwa kunyimwa kushiriki katika Bunge la Katiba kwa sababu tu ya kutokuwa wanachama wa vyama vya siasa.

Tatu, wajumbe 116 wanaopendekezwa kuteuliwa kwenye Bunge la Katiba kwa mujibu wa ibara ya 20(2)(e) na (4) ya Muswada Mpya sio, na hawawezi kuwa, wawakilishi wa wananchi. Kwanza, hawajachaguliwa na mtu yeyote na wala taasisi zao kuwawakilisha katika Bunge la Katiba kwa sababu Muswada Mpya unapendekeza wateuliwe na Rais.

Pili, Bunge la Katiba ni chombo cha uwakilishi wa moja kwa moja wa wananchi na kwa mila na desturi zinazokubalika na kutumika kimataifa, wajumbe wa Bunge la Katiba huchaguliwa moja kwa moja na wananchi bila ya kujali vyama vya siasa na huwa na kazi moja tu: kutunga Katiba Mpya. Kwa sababu zote hizi, Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza wajumbe wa Bunge la Katiba wachaguliwe moja kwa moja na wananchi na kusiwe na masharti yoyote kuhusu uanachama wa vyama vya siasa.

UHALALISHAJI WA KATIBA MPYA

Mheshimiwa Spika, Muswada una mapendekezo ambayo yanaashiria kuachana na utaratibu wa kihistoria wa utungaji wa Katiba ambao umewaweka wananchi kando katika michakato wa kikatiba tangu miaka ya mwanzo ya uhuru. Kwa mujibu wa ibara ya 27(1), kutakuwa na kura ya maoni kwa lengo la kuihalalisha Katiba Mpya. Kwa mujibu wa ibara ya 30, watu wote walioandikishwa kuwa wapiga kura kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya Taifa na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar, watakuwa na haki ya kupiga kura katika kura hiyo ya maoni. Aidha, kufuatana na ibara ya 32(2), matokeo ya kura ya maoni yataamuliwa kwa msingi wa kuungwa mkono kwa zaidi ya 50% ya kura zote zilizopigwa Tanzania Bara na kiasi hicho hicho kwa Zanzibar.

Mapendekezo ya ushirikishwaji wa wananchi katika kuipa Katiba uhai wa kisheria ni jambo la maana sana na linaonyesha kuwa tumeanza kuachana na urithi wa kikatiba wa kikoloni ulioanza na Katiba ya Uhuru ya mwaka 1961.

Hata hivyo, mapendekezo haya yamejaa mitego na vichaka vingi vya hatari. Kwanza, ibara ya 27 inapendekeza kwamba kura ya maoni itaratibiwa na kusimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar. Tume hizi mbili – kwa mashauriano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar - ndizo zitakazotengeneza swali litakaloulizwa kwenye kura ya maoni.

(ibara ya 28(1) na (2) Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 31, utaratibu utakaotumika katika kura ya maoni ni ule unaotumika katika chaguzi za kawaida katika nchi yetu, yaani Sheria ya Uchaguzi wa Taifa, Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar.

Mheshimiwa Spika,
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inarudia kauli yake ndani ya Bunge hili wakati wa kujadili Makadirio na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria tarehe 24 Agosti, 2011: “Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haina imani, sio tu na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, bali pia na mfumo mzima wa kisheria na kitaasisi unaoendesha chaguzi za nchi yetu. Mfumo huu na watendaji wake wameonyesha wazi kutokuwa huru na kutumiwa na Chama cha Mapinduzi kuchakachua matokeo ya chaguzi mbali mbali hapa nchini.

Kwa maana hiyo, Tume ya Uchaguzi ya Taifa, na ile ya Zanzibar, haiwezi kuachiwa jukumu kubwa la kuendesha kura ya maoni kwa ajili ya kupata Katiba Mpya. Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kwamba Serikali ilete bungeni muswada wa mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba na ya sheria husika za uchaguzi kwa lengo la kuiunda upya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha inasimamia zoezi la kura ya maoni kwa uhuru na bila upendeleo kwa chama tawala.”

Kuna maeneo mengine ambayo nayo yanaonyesha kwamba lengo halisi la Muswada huu ni kupata Katiba ambayo haitabadilisha mambo ya msingi ila itakuwa mpya kwa jina tu. Kwanza, ibara ya 26(2) inapendekeza kumpa Rais mamlaka ya “kuliitisha tena Bunge la Katiba lenye wajumbe wale wale siku zijazo kwa ajili ya kutunga masharti ya katiba kabla ya kuizindua Katiba inayopendekezwa kwa lengo la kurekebisha masharti yaliyomo kwenye Katiba iliyopendekezwa.”

Maana halisi ya maneno haya ni kwamba Rais atakuwa na mamlaka ya kuita tena Bunge la Katiba ili lifanye marekebisho ya mambo ambayo yeye au serikali yake au chama chake hawayapendi katika Katiba Mpya kabla haijapigiwa kura ya maoni na wananchi! Kama chombo huru cha wananchi, Rais hawezi kujipa madaraka ya kupingana na kauli ya wananchi kupitia Bunge la Katiba.

Pili, wakati ibara ya 32(3) inapendekeza kurudiwa kwa kura ya maoni endapo kura za ‘NDIYO’ na ‘HAPANA’ zitalingana, ibara ya 32(4) inaelekeza kwamba “endapo wingi wa kura ya maoni utakuwa ni ‘HAPANA’, Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, itaendelea kutumika.” Endapo pendekezo hili litapitishwa na kuwa sheria, hii itakuwa ni kualika maasi kwa vile, kwa vyovyote vile, wananchi wa Tanzania – baada ya kupitia mchakato mrefu wa kutengeneza Katiba Mpya – hawatakubali tena kuvishwa minyororo ya Katiba ya sasa.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba badala ya kurudi kwenyestatus quo ante kama inavyopendekezwa, mchakato wa Katiba Mpya uanze tena hadi hapo utakapopatikana muafaka wa kitaifa wa katiba.

HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, 2011 ni Muswada muhimu kuliko pengine miswada yote ambayo Bunge la Kumi litapata fursa ya kuijadili na kuipitisha. Ni muswada wa kihistoria kwa vile, tangu uhuru wa Tanganyika miaka hamsini iliyopita, na tangu Muungano miaka karibu arobaini na nane iliyopita, Watanzania hatujawahi kupata fursa ya kujadili na kuamua mustakbala wa taifa letu kikatiba kwa utaratibu kama unaopendekezwa katika Muswada huu.

Hata hivyo, kwa jinsi ambavyo Muswada huu ulivyoandaliwa na kwa maudhui yake na kwa jinsi ulivyoletwa Bungeni kwa kukiuka makusudi Kanuni za Bunge, ni wazi – kama utapitishwa jinsi ulivyo – Watanzania tutakuwa tumekosa fursa ya kuamua mustakbala wa taifa letu kwa njia ya amani na maridhiano.

Bunge hili tukufu lina wajibu mbele ya historia na kwa vizazi vya sasa na vijavyo, kuhakikisha kwamba tunapata muafaka wa kitaifa juu ya Tanzania tunayoitaka. Hukumu ya historia, endapo Bunge hili tukufu litaendekeza ushabiki wa kisiasa na kufanya maamuzi ya mambo makubwa kama haya kwa kupiga kelele au kwa kuzomea au kwa kugonga meza kwa nguvu, itakuwa ni kali sana.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haiwezi kuwa sehemu ya maamuzi makubwa kama yanayopendekezwa na Muswada huu bila kwanza wananchi wa Tanzania na Wabunge wenyewe kupata muda wa kutosha wa kuyatafakari masuala haya yote kwa uzito unaoyastahili na kuyafanyia maamuzi ya busara.

Kwa sababu hizi zote, Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja chini ya kanuni ya 86(3)(b) ya Kanuni za Kudumu za Bunge hili tukufu kwamba Bunge hili likatae Muswada huu Kusomwa Mara ya Pili kwa sababu Serikali imeleta Muswada Mpya na wenye mabadiliko makubwa na ya msingi bila kufuata masharti ya kanuni ya 84(3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge; na pia kwa sababu Serikali haijatekeleza maagizo ya Bunge hili tukufu kuhusu kutoa muda zaidi kwa Kamati na wananchi kuufikiria, kuuelewa na kuutolea maoni Muswada huu kinyume na matakwa ya ibara ya 18(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano juu ya uhuru wa wananchi kutoa maoni yao; ibara ya 21(1) na (2) juu ya haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wan chi, na haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayowahusu wananchi, maisha yao au yanayolihusu Taifa.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
---------------------------------------------------------------
Tundu Antiphas Mughwai Lissu (MB)
MSEMAJI, KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI & WAZIRI KIVULI, KATIBA NA SHERIA

Monday, November 14, 2011

Bi Mkora Alonga Toka Msamvu: Denti Bongo Ana Babu Wa ATM, Denti Mwenzie Wa KuDessa Na Wa Moyoni Mtaani!



Mdau umenena vyema ila umekosea pale ulipoweka percentage kwa sababu hujafanya utafiti uliokupa hiyo data, ungeishia tu kwenye wanawake wengi wana tabia hizo. Huko nyuma nilishawahi kuliongelea hili suala lakini hasa lilihusu wanawake wanaokataa kuolewa na vijana wenzao na kwenda kutembea na waume za watu ambao wamekwishajijenga tayari. Wanasahau kuwa hao waume za watu walikuwa supported na wanawake wenzao mpaka wakafikia kusimama hapo walipo kuwa wenye uwezo wa kuwanunulia magari na kuwajengea majumba au kuwapangia nyumba maeneo ya bei mbaya kama Masaki, Osterbay, Upanga, Mikocheni na Msasani. Wanasahau usemi wa ukiona vinaelea ujue vimeundwa.

Na kwa wanafunzi wa vyuo siku hizi hali ni mbaya wewe unazungumzia huko ughaibuni lakini hata hapa kwetu Bongo ndio inazidi. Wanafunzi wa kike utakuta ana baba mtu mzima mwenye mke na watoto huyu yeye ni ATM tu ya kuhakikisha ana pesa ya kutumbua na kujifanya mutoto wa mujini; kisha ana mwanafunzi mwenzie wa kumpa madesa (sijui siku hizi mnaitaje)huyu kazi yake kumfanyia assignment za shule, kumbuka yeye hana muda wa kufanya assignment kwa sababu yuko busy na biashara ya wanaume na sio kama uwezo huo hana hapana tatizo ni muda. Na mwisho anakuwa na kijana wake anayempenda kwa dhati na ikitokea huyo kijana hajagundua huu mzunguko basi ndio atakayemuoa la akimgundua basi ataishia mtaani.

Na akifika kazini trend ni ile ile pale ofisini atakutana na waume za watu ambao wana pesa za kumwezesha kuendelea kuishi yale maisha yake artificial aliyotoka nayo chuoni, na matokeo yake msichana mwenyewe anakuwa amejifunga kwenye kamba ambayo inamfanya asipate mume wa kumuoa. Hii wasichana wengi hawaijui kwa sababu jinsi wanaume walivyo wakikuona tu unatembea na mume wa mtu basi wewe sio tena wifey materials kwa sababu unaonekana hudhamini ndoa na yeye anaogopa akikuoa utakuja kuisaliti ndoa.


Na zaidi kinachopelekea kuongezeka kwa hayo mambo ya tamaa ni hizi social networks sijui Facebooks na mablogu ambayo wasichana kupeleka mapicha yao ya kuringishiana nani ana amevaa designer's outfit nani anaendesha gari ya kifahari na nani anakaa kwenye mtaa wenye address inayoeleweka, kiujumla ni kama kuna mashindano ya punda na farasi.

Na hao wadada wajameni hawana haja ya kuwaonea wivu mnapokuwa mmeoa wazungu wenu kwani mmetoka mbali kwa shida na raha, mmelala kwenye kachumba kadogo bila heating, mmekula noodles za kupika kwenye microwave, mmekunywa kahawa cheap ya kwenye thrifty shops au 1 pound shop. Sasa ukifika wakati wa hao wadada wa kizungu kula matunda ya kazi yao wao kinawauma nini? Wakiona vimeelea wajue vimeundwa, wakati wenzao walipokuwa wanaunda maisha na nyinyi wao walikuwa wanakula dezo ya vilivyoundwa na wanawake wenzao kwa kutembea na wababa wakubwa waume za watu. Kwa kifupi wamevuna walichopanda na majuto ni mjukuu, wasichana wengi wanasahau kuwa kwa mwanamke kila dakika inayopita na biological time is also ticking.

Kwa kumalizia tu zamani haya yalikuwa zaidi yanafanywa na wanawake lakini siku hizi ni maendeleo hata watoto wakiume wanaopenda dezo hutoka na mijimama mikubwa na kubaki wakiitwa "Serengeti boys". Hili nitaliongelea siku nyingine panapo majaliwa nikipata ka umeme ka kuwasha kwenye komputa yangu huku Msamvu.

chanzo cha habari ni Mjengwa Blog