CONTACT US:

CONTACT US:
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com

Wednesday, December 8, 2010

TABIA ZA WANADAMU NA USHAURI WAKE


Zipo tabia asili nne (4)za mwanadamu nazo ni kama zifuatazo
1:TABIA YA SANGUINE:

(a)ni mcheshi, (b) Amejaa tabasamu,(c)Nimwenye huruma sana,(d)Yeye hutizamia mema tu (e) ni mkarimu (f)hakosi neno (g)ni mwepesi kufanya urafiki na mtu na ana marafiki wengi,(h)ni msemaji sana(i)ni mfanya biashara(j)ni daktari mzuri.
UDHAIFU ALIONAO SANGUINE
Ingawa sanguine ana sifa nzuri nyingi lakini anao udhaifu ufuatao:-
(a)Ni mropokaji sana, (b)Urafiki wake ni wa pale yupo tu akiondoka anasahau, (c)Si mtunza siri,(d) Ni malaya, (e) anapenda kula (f)Haishi utoto,(g)Si mtawala. Kwa hiyo yeye ni rahisi kwake kupoteza umaarufu wake haraka maana hana "pazia"

2:TABIA YA CHOLERIC

Sifa za mtu huyu ni:
(a)Ana maneno kiasi (b)Ni mtu wa kazi (c)Nikiongozi wa kuzaliwa (d)Maisha kwake ni kazi tu (e)Ni mwenye nguvu (f)Mara nyingi hufanikiwa kwa sababu hawakati tamaa upesi-ni watu wa kusonga mbele sio watu wakutishwa kwa urahisi hapendi kuonewa au kuona jambo likiharibika, hivyo hawangoji kamati au mkutano.
UDHAIFU WAKE CHOLERIC
(a)ni mtu mwenye hasira sana,(b)Ni mgomvi,mkali, (c)ni mkatili na hata ukorofi wanao.

"ITAENDELEA KESHO"

No comments:

Post a Comment