CONTACT US:

CONTACT US:
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com

Friday, October 21, 2011

FAMILIA MASKINI ILIYOKALIA UTAJIRI BILA KUJUA MKOANI MORO


Mawe yakiwa nyuma ya nyumba hiyo yakiashiria kuwepo kwa madini katika eneo hilo.


Pichani ni nyumba na familia ya Ally wakionekana kuwa na furaha na amani.
http://www.blogger.com/img/blank.gif
USILOLIJUA sawa na usiku wa giza. Mwenye nyumba hii kijiji cha Melela-Mlandizi, Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro, ambaye mtandao ulipata jina lake moja tu la Ally, ameishi miaka mingi eneo hili bila kujua kwamba lina utajiri mkubwa wa madini ya dhahabu.

Hivi sasa eneo hilo limevamiwa na wachimba dhahabu kibao kutoka sehemu mbalimbali nchini, hususani Mkoa wa Morogoro. Isitoshe, matajiri wengi kutoka Dar es Salaam walikutwa na mtandao huu wakikagua eneo hilo ili kuyafikia madini hayo yenye thamani.

Juhudi za kuzungumza na mmiliki wa nyumba hiyo, ziligonga mwamba baada ya familia yake kusema alikuwa mbali.

HABARI/ PICHA NA DUNSTAN SHEKIDELE, /GPL, MOROGORO

No comments:

Post a Comment