CONTACT US:

CONTACT US:
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com

Monday, October 24, 2011

MWANAMKE AFUKUZWA NA MUMEWE NDANI YA NYUMBA ARUSHA


Jennifer Dunistar akiangua kilio wakati akiongea na mwandishi wa habari hii.


Nyumba ambayo Jeniffer alikuwa akiishi na mumewe ambayo imepangishwa na kumfanya akose mahali pa kuishi.

Na Joseph Ngilisho, Arusha
MWANAMKE, mkazi wa Kimandolu katika Jiji la Arusha, Jeniffer Dunistar (35) anaishi katika mateso makubwa yeye na mtoto wake mdogo baada ya mume wake wa ndoa Dunistar Ng’unda (39) kumfukuza ndani ya nyumba waliyokuwa wakikaa na kuipangisha kibabe.

Akizungumza kwa uchungu huku akitokwa machozi ,Jeniffer ambaye ana watoto watatu aliozaa na mwanaume huyo, alisema sasa anaishi kwenye kibanda yeye na mtoto wake wa miaka mitatu na hana msaada wowote kwani nguo anazotumia amekuwa akigawiwa na Wasamalia Wema wanaomwonaea huruma wakati akihangaika.

Mwanamke huyo alisema mumewe aligawa vitu vyake vyote wakati akiwa hayupo.

Alisema kuwa mwanaume ambaye alianza kubadilika tabia baada ya kujiunga na kanisa la Walokole la The Pool of Siloam, na amegawa vitu vyake mbalimbali kwa hawara yake na kuitelekeza familia yake.

Jeniffer alisema mumewe alimdanganya kwamba nyumba hiyo ilikuwa ni ya urithi, yaani ya baba yao, lakini alipokwenda kumuuliza mkwewe (baba wa mumewe) alikataa na kusema haijui nyumba hiyo.

Miongoni mwa manyanyaso ambayo mwanamke huyo ameyapata ni http://www.blogger.com/img/blank.gifpamoja na kupigwa kila mara na Dunistar.

Akifafanua, alisema walifunga ndoa mwaka 2003 na kuanza maisha wilayani Simanjiro na baadaye kununua nyumba hiyo iliyopo eneo la Kimandolu na kuishi kwa pamoja zaidi ya miaka saba na kufanikiwa kupata watoto watatu, ambapo mtoto wa kwanza ana umri miaka kumi.

Jeniffer amefungua kesi ambayo inaendelea kuunguruma kwani kila akidai talaka mumewe amekuwa akikataa.

Inadaiwa Dunistar ana nyumba zaidi ya tano walizojenga na mke wake huyo zilizopo mjini Arusha huku katika

HABARI KWA HISANI YA GLOBAL PUBRISHERS

No comments:

Post a Comment