WABUNGE WA UJERUMANI WAMGOMEA POPE BENEDICT XVI !
WATOKA NJE YA BUNGE !
Heti siasa na dini ni sawa kuchanganya maji na mafuta katika chupa ?
Wengine wanadai kisa kupingwa kwa kondomu !
Kweli Nabii hana utukufu nyumbani kwao !?
Kiongozi wa kidini wa kanisa la Kikatoliki duniani Mtakatifu Pope Benedict xvi (Joseph Ratzinger),amejikuta
yupo katika mvutano mkubwa na wanasiasa nchini ujerumani,baadhi wabunge wapatao 100
wametoka nje ya bunge la ujerumani wakati Pope Benedict akiwa analihutubia bunge la nchi
hiyo (Bundestag) majira ya halasiri ya alhamisi 22-09-2011 mjini Berlin,ambako Baba mtakatifu
yupo ziarani nchini ujerumani! wabunge hao wamemsusia Pope na kutoka nje ya bunge ambako walijumuhika na
waandamaji wa wengine waliokuwa wanampinga Pope kuwepo katika ukumbi wa bunge hilo!
Habari za uhakika zinaeleza kuwa baadhi ya wanasiasa na wabunge nchini ujerumani hawakubaliani
na taratibu za uongozi wa Pope ,haswa linapokuja swala la matumizi ya KONDOMU,kwani kanisa
la kikatoliki halikubaliani na matumizi ya kondomu,pia sababu zingine za kupingwa kwa Pope nchini ujerumani
ni pamoja kashifa zinazowagusa baadhi ya watumishi wa kanisa la kikatoliki
duniani kwa kuhusika na kuwafanyia vitendo vichafu watoto au vijana katika miaka ya nyuma.
Pope Benedict amekuwa muwazi na amewahi mara nyingi kuomba radhi hadharani kwa niaba ya
kanisa lake,lakini wakosoaji bado wanaendeleza nongwa ! sababu nyingine ya wanaopinga kulihutubia bunge la
ujerumani ni kuwa DINI NA SIASA ni vitu viwili tofouti kwa maana hii
Pope Benedict xvi (Joseph Ratzinger) hapaswi kuhuwepo ndani ya jumba au kulihutubia bunge
ambalo ndilo baraza la kutunga sheria.
Pope Benedict xvi ni mzaliwa wa ujerumani,alizaliwa kwa jina la Joseph Ratzinger ,huko Bayern, ujerumani ya kusini.
Vyombo vya habari nchini ujerumani vimetonya kuwa kuanzia mwaka 2010 wafuasi wapatao 160,000 wa kanisa la kikatoliki
nchini Ujerumani wamelihama kanisa hilo na kujiunga na madhehebu mengine.
No comments:
Post a Comment