CONTACT US:

CONTACT US:
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com

Tuesday, November 22, 2011

AFISA USTAWI WA JAMII KOROGWE APONGEZWA

Mhariri,
SINA shaka na kujitokeza kwangu hadharani kupitia gazeti hili kutoa maoni yangu kwa nia ya kumshukuru na kumuenzi afisa ustawi wa jamii wilayani kwetu, Korogwe, Tanga.

Kwa hakika ni kwa jinsi ambavyo anatumikia jamii tangu nilipoanza kumuona, yapata miaka kumi iliyopita.
Kama tunavyofahamu, majukumu ya ustawi wa jamii katika kusimamia, kuelekeza na kuhakikisha malezi ya watoto yanakidhi kiwango hasa kwa wanandoa/ marafiki wanapohitirafiana, kuhusu suala zima la matunzo ya watoto, ni kazi nzito.

Imekuwa kama kawaida kwa sisi hasa kina baba kuwaachia mzigo mkubwa wa malezi kinamama kwa visingizio vingi.
Baadhi ya kina mama waelewa hukimibilia katika idara hii, ndipo ninapommiminia sifa lukuki afisa huyu kwa ushahidi ufuatao.
Wakati mmoja mwaka 2004, nilishuhudia kisa kimoja cha afisa wa serikali tena katika taasisi nyeti sana, mwenye cheo kikubwa alipopelekwa kwake na mama ambaye ni mkazi wa kijijini kwetu.

Afisa huyu hakujali cheo kikubwa cha mwanaume huyo wala uwezo wake wa kifedha, alisimama kidete kutetea haki za mwanamke na mtoto husika mpaka wakatendewa haki kwa mujibu wa taratibu.

Ni mengi amefanya ofisa huyo, si vyema kutomshukuru angalau kwa njia hii, ili kumtia moyo aendelee kufanya hivyo kwa wengine wenye matatizo kama hayo huku akifahamu kuwa jamii iliyomzunguka ipo pamoja naye, na inamkubali.

Naamini viongozi wengine hawana budi kuiga kwa utendaji wa kazi wa ofisa huyo na wote wangekuwa hivi tungekuwa mbali kimaendeleo na katika kuondoa kero za wananchi.

CHANZO MWANANCHI Friday, 18 November 2011 09:25

No comments:

Post a Comment