CONTACT US:
CONTACT US:
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com
Monday, November 21, 2011
UMASIKINI WA TANZANIA NA MAENDELEO MABOVU YA ELIMU
SHULE ya Msingi Kitete iliyopo katika kata ya Uchindile, Tarafa ya Mlimba wilayani Kilorombero mkoani Morogoro yenye walimu wawili tu na wanafunzi 29 ipo katika mazingira yanayoashiria imetelekezwa.
Shule hiyo iliyoanzishwa kwake mwaka 1976 ipo zaidi ya kilomita 150 kutoka Kilombero na kilomita zaidi ya 125 kutoka Mafinga, mkoani Iringa.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Idd Mdaba alisema tangu ahamishiwe katika shule hiyo mwaka 2008 kwa ahadi kwamba angehamishiwa shule nyingine baada ya miaka mitatu, amekuwa akifundisha mwenyewe wanafunzi wa madarasa yote yaliyopo katika shule hiyo.
“Hata hivyo nashukuru mzigo huo umepungua mwezi mmoja tu uliopita baada ya kuletewa mwalimu mwingine mmoja kutoka wilayani Geita ,” alisema huku Mwalimu huyo Juma Deke akidai kujutia uamuzi wa kuomba uhamisho kutoka Geita ili ahamie mkoani kwake Morogoro kwani hakujua kama angepangiwa shule kama hiyo.
Alisema mbali na shule hiyo kutokuwa na vifaa vya kufundishia na kujifunzia, ofisi ndogo ya mwalimu na madarasa yake matatu yaliyopo, hayajasakafiwa chini na kuta zake, hakuna madirisha na milango na yote kwa ujumla wake yana madawati yasiozidi 20.
Mdaba alisema mazingira hayo yameifanya shule hiyo kukosa wanafunzi wa darasa la kwanza, la tatu na la tano hadi la saba hivi sasa baada ya waliopaswa kuwa wanafunzi wa madarasa hayo kutosajiliwa mwaka wa kwanza wa masomo yao ya darasa la kwanza
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kitete iliyopo katika kata ya Uchindile wilayani Kilombero, Idd Mdaba akitoka kwenye ofisi yake kama anavyoonekana.
Source:Frank Leonard
Hili ni moja ya darasa la shule ya msingi Kitete iliyopo kata ya Uchindile wilayani Kilombero linavyoonekana kwa ndani. Shule hii ina walimu wawili na wanafunzi 29 tu kwasababu ya mazingira yake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Tanzania sio maskini. Ni ubovu na kukosa uadilifu, uzalendo na uoga kwa watendaji. Kila mtu anaubinafsi, akipata upenyo anajichukulia mapema na maendeleo hayatapatikana kwa mtindo huu... pesa zinatoka sana hasa ukiangalia 'misaada' inayotolewa na mashirika na makampuni mbali mbali. leo hii tungepiga hatua fulani laiti watendaji wangekuwa waaminifu na wacha MUNGU..
ReplyDelete