familia hii ina hatari ya kutoweka kutokana na ongezeko la mauaji ya albino yanayo endelea nchini.
swali la kujiuliza ni kuwa wako wapi maafisa ustawi wajamii katika vita ya mapambano dhidi ya mauaji ya albino? sijapata kusikia toka kwa kamishina wa ustawi wa jamii wala maafisa ustawi wa wilaya hata kwa wana taaluma walioko vyuooni wakikemea suala hili.
kama haitoshi ungekuwa ni muda muafaka kwa wana ustawi kuonyesha umuhimu wa taaluma yenu na nini mna kifanya kwani kama mgefanikisha kuyakomesha mauaji haya basi mgeitangaza taaluma yenu kwa kiasi kikubwa sana katiaka jamii.
naomba kuwasilisha. (mdau sadath)
No comments:
Post a Comment