MAJUKUMU YA IDARA.
- katika kuendeleza, kutetea na kulinda haki za watu wenye ulemavu na wazee, idara inaongozwa na sera na sheria zifuatazo:
- sera ya taifa ya maendeleo na huduma kwa watu wenye ulemavu.
- sera ya taifa ya wazee.
- sheria za ajira na matunzo kwa watu wenye ulemavu Na.2 na 3 za mwaka 1982.
2: katika kuendeleza, kushawishi na kulinda haki na ustawi wa familia, watoto yatima na walio katika mazingira magumu zaidi pamoja na kusimamia vituo vya kulelea watoto mchana, idara inaongozwa na sheria na miongozo ifuatayo:
- sheria ya makao ya watoto Na. 4 ya mwaka 1968.
- sheria ya vituo vya kulelea watoto wadogo mchana Na. 17 ya mwaka 1981.
- mwongozo wa malezi ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu zaidi.
3: katika kurekebisha, kulinda haki za watu na watoto walio katika mkinzano wa kisheria, idara inaongozwa na sheria na miongozo ifuatayo:
- sheria ya majaribio na ujenzi wa tabia sura 247 ya mwaka 1947.
- sheria ya watoto na vijana sura ya 13 ya mwaka 1937.
- mwongozo wa huduma za majaribio na ujenzi wa tabia.
No comments:
Post a Comment