
somo; vizuizi mimba
mada: kondomu ya kiume.
lengo: baada ya kipindi hiki kila mmoja wetu aweze kueleza kwa ufasaha jinsi kondomu inavyotengenezwa, kazi yake, inavyokosa kazi na inavyoingilia na kuvuruga kiini cha ndoa.
a. aina ya kondomu
kuna kondomu za aina mbili
1. kondomu iliyo tengenezwa kwa kutumia mipira -latex condom.
2:kondomu iliyo tengenezwa kwa ngozi ya mnyama - animal skin membrance condom. hii haina uhakika katika kuzuia ukimwi na magonjwa mengine.
b. utengenezaji wa condomu.
*kondomu hutengenezwa kwa kuunganisha ngozi mbili nyembamba za mpira ili matundu ya ngozi *layer* yazibwe na layer ya pili na yale ya layer ya pili yazibwe na layer ya kwanza . ukubwa wa matundu *natural pores* ni kipimo cha micron 5 wakati ukubwa wa kirusi cha ukimwi ni micron 0.5 (washington times,april 22,1992)
*utengenezaji wa kondomu hufanyika katika mazingira ya ubaridi ili kuhifadhi uimara wa mpira. baada ya kutengeneza kondomu kwa kuunganisha layer mbili (doubledipped) ni lazima ipimwe kwa darubini maalumu iitwayo scanning electronic microscope (sem) iwapo bado matundu yanaonekana ambayo pia hutoa picha ya kondomu iliyotanuliwa (2000+magnification) (from the surgeon general, us public health - jama june 1, 1993 pg. 2,840).
*kisha kondomu huwekewa dawa ya kuhifadhi isiharibike *lubricants* na kufungwa kwenye maboksi. iwapo maboksi haya yatauzwa ulaya au amerika hubandikwa karatasi zinazomuelekeza mtumiaji kuwa asiweke tumaini katika kondomu kwa kuwa haziwezi kumkinga asiambukizwe virusi vya ukimwi. iwapo kondomu hizo zitauzwa nchi maskini hakuna angalisho linalowekwa kwenye maboksi hayo. kama maboksi hayo yatasafirishwa hadi dar es salaam, tanzania, yatawekewa nembo inayooonyesha na kumpa matumaini mtumiaji wa kondomu kuwa ni kinga kamili dhidi ya kuambukizwa virusi vya ukimwi.
*maboksi ya kondomu yakitolewa kiwandani kwenye ubaridi hupakiwa kwenye meli na kuanza safari ya zaidi ya miezi sita kupitia baharini yakikumbana na hali ya joto ndani ya makontena. joto huathiri uimara wa mpira (uimalishaji wa familia uk.148)
c. matatizo ya kondomu
1. kukosa kazi yake mara nyingi (failure rate)
sababu
a.vitundu vidogovidogo (pores) kama ilivyo katika kila aina ya mpira. wakati wa kutumia kondomu ipo nguvu ya msukumo au mkandamizo (pressure stress), mpishano wa layer za kondomu (twisting stress), msuguano wa mpira kati ya watu wawili (mechanical and friction stress) na kusababisha kondomu kuchunika na hatimaye kondomu kulika kutokana na mchanganiko wa dawa ya kuhifadhi kondomu na tindikali ya uke (std july-agust 992 pg. 230-23).
b. kutoka wakati wakufanya tendo la ndoa.
c. kupasuka wakati wa kufanya tendo la ndoa.
d. kuyeyuka wakati wa joto.
2. inaingilia kiini cha ndoa na kuvuruga umoja wa umoja wa miili, yaani tendo la ndoa.
a. inasababisha maumivu kwa wanawake wengine kwa sababu ya msuguano kati ya kondomu na ukuta wa uke. lengo la umoja wa miili la kumpa mwenzake furaha halikutimizwa, bali limeleta maumivu.
b. inabidi kufuata kanuni kumi juu ya namna ya kutumia kondomu, ili iweze kufanya kazi yake. hii inasababisha mume kuifikiria sana kondomu wakati wa tendo la ndoa. hii inamzuia kuwa na umoja wa roho na umoja wa mioyo na mke wake na pia inamzuia kumsaidia mke wake kufikia msisimko shirikishi. hii inamdhuru sana mama katika moyo. pia mume mwenyewe anahangaika na kondomu,wanashindwa furahia tendo la ndoa.
c. inazuia mwanamke kutambua siku za uzazi na zisizo za uzazi. msuguano (friction) kati ya kondomu na ukuta wa uke unasababisha kutoka maji kwenye ukuta wa uke (transudat). kwa hiyo kila siku mwanamke anaona aina ya maji maji aoni ukavu.
d. kondomu maranyingi inatumika kabla ya ndoa na nje ya ndoa. kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa ni dhambi. mungu amesema usizini . ukifanya tendo la ndoa nje au kabla ya ndoa na kondomu au bila kondomu ni dhambi sawa sawa. tendo hili uitwa pia uasherati, umalaya, ukobe. ni sawa ukifanya na kondomu au bila kondomu. kwa hiyo ni dhambi. dhambi inamtenganisha mwanadamu na mungu.
e. maadili: lengo la kupanga familia na kuzuia vijidudu kutuletea magonjwa na kifo ni vizuri na linafaa. cha muhimu ni aina ya njia. kuhusu kondomu, uhakika wake ni mdogo, tena inaleta madhara ya mwili (maumivu kwa mwanamke) na madhara ya kiroho (kutoridhika umoja wa miili),kumtenganisha na mwenzake na mungu. kwahiyo lengo halihalalishi njia: the end does not justify the means.
f. njia iliyo bora ni billings.
imetolewa na ufata umoja wa familia tanzania.
No comments:
Post a Comment