CONTACT US:

CONTACT US:
Mobile : 0755 484866
EMAIL : socialworkertz@yahoo.com

Saturday, August 7, 2010

KUMSAIDIA MTOTO OMBAOMBA SIO KUMPA FEDHA




JUU PICHANI NI MSANII KANUMBA AKIWA NA JB PAMOJA NA MTOTO WALIYE MPATIA MSAADA

kabla sijaianza mada yangu niwashukuru kanumba na JB kwa kuguswa na kuamua kumsaidia huyo mtoto. sasa nirudi kwenye mada kwa kuanza na kunukuu maneno aliyo yatoa muandishi toka kwenye blog ya RAY THE GRETEST alisema hivi "Kuna kitu kilinisikitisha sana baada ya kutoka nje ya uwanja,Mtoto huyu anaishi na virusi vya ukimwi baada ya kuambukizwa na mzazi wake tumboni anaishi kwa kuomba misaada kwakweli nilimwonea huruma sana ikabidi nitoe kiasi cha pesa fulani mfukoni na kumkabidhi naye alishukuru sana na kuanza kutuombea kwa mungu"
Mwisho wa kunukuu nisawa ila mlipaswa kujiuliza kwanini huyo mtoto anishi na virusi vya ukimwi harafu yuko hapo bila mtu wa kumsaidia hata kumkumbusha muda wa kumeza dawa unapofika, pili je ni kweli huo msaada mliompa utamsaidia au utaishia kwa vijana wenye nguvu zaidi yake kwa kumdai ujira wa alicho kusanya siku hiyo?

mimi nilikuwa napenda kuwashauri watanzania wenzangu kuwa tunapotaka kuwasaidia watu wenye shida hasa watoto lazima tufanye utafiti na kujiridhisha kuwa huyu mtoto tunaye msaidia atanufaika na msaada wetu kwa mfano mtoto waliye kutana naye akina kanumaba ingebidi wamuulize yule mtoto historia yake kwa ufupi ikiwa ni pamoja na kujua mtu wake wakaribu ambaye wangeenda kuongea naye na wakaangaia wamsaiidieje huyo mtoto ikiwa ni pamoja na kuwashauri hao ndugu wa karibu wa huyo mtoto kumpeleka hospital ama kwa mshauri ili aweze kusaidia kumjenga huyo mtoto kisaikolojia jambo ambalo linge fanikisha kurudisha afya ya mtoto huyo. narudia tena hawakufanya vibaya kumsaidia huyo mtoto ila walipaswa kuangalia na nini chanzo cha tatizo. kwa kufanya hivi tutaisaidia jamii yetu kuondokana na tatizo la watoto wa mitaani kwani kwa kuishia kuwapa pesa na kuondoka ni sawa na kuwaita waongezeke maana wanapata pesa ambayo na sawa na mshaara kwao.
NAKARIBISHA HOJA.

No comments:

Post a Comment