PICHA KWA HISANI YA USTAWI WA JAMII TANZANIA
Taifa hili linakadiriwa kuwa na watu wapatao 42 milioni, lakini haina hata hospitali moja ya rufaa ya watoto. Sijasema haina hospitali zenye wadi za watoto au hakuna vitengo vya watoto katika hospitali zilizopo, la hasha! Hakuna hospitali ya taifa ya kuhudumia watoto.
Hakuna hospitali ya watoto waliochini ya miaka 18; hakuna hospitali inayotoa huduma yoyote inayohusiana na magonjwa ya watoto na masuala yanayohusiana na watoto.
Ni muhimu kuwa na hospitali maalum zinazoweza kuhudumia watoto, kutokana na uwepo wa magonjwa mbalimbali yanayowasumbua watoto zaidi na pia mahitaji ya kitabibu kwa watoto.
Umuhimu wa kuwapo kwa hospitali japo mbili za rufaa za watoto umeonekana zaidi katika matukio makubwa mawili ya karibuni na yanayoshabihiana. Matukio ya milipuko ya mabomu kule Mbagala na hili la juzi huko Gongo la Mboto.
Kwa mtu yeyote ambaye alifuatilia matukio ya Gongo la Mboto atakuwa ameona ni jinsi gani changamoto kubwa sana ilikuwepo katika kuhudumia watoto.
Habarii imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la Mwanahalisi la tarehe 16/03/2011, iliyo andikwa na M. M. Mwanakijiji, kichwa cha habari kilikuwa kinasomeka hivi NSSF iachane na Kiwira.
No comments:
Post a Comment